Kama Una Tabia Hii, Jua Kwamba Unakosa Kitu Hiki


Kuna kitu huwa kinanishangaza, mtu anakuwa na pesa ila anasema ngoja niiweke weke  tu kwenye nguo. Au vitabu vyangu.
Siku nikikutana nayo na sina pesa pesa nitafurahi.

Mtu anaweka pesa yake ovyo ovyo, eti siku akivaa nguo akakutana nayo bahati mbaya basi atafurahi.
Au anasubiri siku akipigika ndio anaanza kufurumusha nguo zake aangalie kama kuna pesa.

Je, umewahi kuwa na tabia hii.
Kama umewahi kuwa na tabia hii basi hauna NIDHAMU. Hauna nidhamu ya kutunza pesa.
Hauna nidhamu ya kukaa na pesa.

Na tabia hii haitaweza kukufikisha kwenye mafanikio makubwa. Badala yake itakuangusha.

 Unapaswa kuwa na nidhamu ya kutunza pesa. Moja ya tabia ya kikomavu ni uwezo kukaa na pesa, bila kuitumia.
Hii ni tabia ya watu waliokomaa.

Hivyo unapaswa kujifunza tabia hii kila iitwayo leo.  Na ili uwe na tabia hii basi unahitaji nidhamu

Soma Zaidi: Hivi Ndivyo Unapaswa Kuishi Maisha Yako

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X