Kitu Hiki Ndicho Kinapaswa Kukusukuma Kuwa Kiongozi


Kwanza kabisa napenda nikwambie kwamba wewe ni kiongozi.

Haijalishi kwamba unafanya kazi ya kufagia, au wewe unadeki ofisi fulani. Wewe ni kiongozi.

Ufahamu Ufalme Wa Mteja Na Jinsi Ya Kumhudumia
Mwananchi, septemba 27 2018

Haijalishi unafundisha wanafunzi wa awali tena chini ya uongozi wa mtu fulani. WEWE NI KIONGOZI

Haijalishi wewe ni mjasiliamali, umeajiriwa, umejiajiri, umefukuzwa kazi unasoma, umehitimu, n.k
Narudia tena WEWE NI KIONGOZI

Kumbuka kwamba uongozi sio lazima uwe na cheo au madaraka.

Uongozi sio lazima uwe na watu waliokuznguka na bunduki. Wala uongozi sio lazima ukipita mahali watu wainame na kusema mheshimiwa.

Soma Zaidi:  Hii Ndiyo Sifa Ambayo Kila Kiongozi Anabeba

Kama ulikuwa unaelewa hivyo uongozi naomba ufute hiyo maana. Maana hapa kuna maana mpya ya uongozi.

Ni uwezo wa kuongoza watu bila ya wewe kuwa na cheo!  Madaraka huja, madaraka huondoka lakini uongozi hauondoki!

Ukishakuwa kiongozi unakuwa kiongozi maisha yako yote. Sasa ule uwezo wako wa kufanya kazi kwa ubora na kwa viwango vya vya juu, ndio tunauita uongozi,

Huhitaji cheo kufanya kazi kwa viwango vya kimataifa.
Huhitaji cheo au madaraka kujituma
Huhitaji cheo kufanya kazi bila kuambiwa au kusimamiwa.

Sasa kama wewe ni kiongozi kuna kitu kinapaswa kukusuma, na kitu  hiki sio kingine bali ni KUTUMIKIA.

Sifa ya uongozi ni kwamba, ukianza kuwa kiongozi kwenye ngazi uliyopo sasa, utapata wafuasi.

Kwa hiyo watakuwepo watu wanakufuata nyuma yako.
Kwa hiyo utapaswa kuendelea kuonesha njia, ili wafuasi wako wanufaike zaidi.

Sasa, wewe kama kiongozi kuna vitu havipaswi kukusukuma kuwa kiongozi.

Unapaswa kusukumwa na KUTUMIKIA.
penda kutoa huduma kwa watu zaidi ya unavyopenda kitu kingine.

Usisukumwe na kupata pesa zaidi maana pesa huja na pesa huondoka. Lakini kama utatoa huduma utaacha alama ambayo ni kubwa sana.

Wala usisukumwe na kupenda  madaraka.

Wala hata  usisukumwe na kutaka sifa. Sukumwa na KUTUMIKIA WATU.

Viongozi wote hata kama wana vyeo, wakisukumwa na kuhudumia watu, huwa viongozi wazuri sana kwenye dunia hii hapa.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X