Maswali Matatu (03) Unayopaswa Kujiuliza Kabla Ya Kuanza Safari


Kati ya vitu ambavyo watu hawapendi ni maswali.
Ukiwa darasani wanafunzi hawapendi kuuliza maswali lakini pia walimu hawapendi kuulizwa maswali na kinyume chake ni sahihi!

Lakini maswali kwa kawaida ndio huja uvumbuzi, ubunifu na mambo mapya.

Ona mtu kama Newton, baada ya kuona tunda linaanguka chini alijiuliza swali kwa nini lianguke chini badala ya kwenda juu. Swali hili ndilo siri iliyonyuma ya ugunduzi wa sheria ya uvutano.

Nakumbuka siku moja wakati nasoma kitabu cha YOU HAVE A BRAIN cha Ben Carson, mwandishi alikuwa anasema hivi,
Mama yake alikuwa na utaratibu wa kumuuliza swali pale alipokuwa anakosea, alikuwa akimuuliza hivi “Ben mwanangu unao ubongo”?
Ben Carson anasema swali hili lilikuwa linamfanya afikiri sana, na ndilo lilimfanya kuwa alivyo. Kumbe maswali yanatujenga. Iwe tunajiuliza wenyewe, tunauliza au tunaulizwa na watu.
Hatupaswi kuyakimbia maswali maana maswali ndio chanzo cha ukuaji, ubunifu, uvumbuzi n.k

Sasa hapa nimekuwekea maswali matatu muhimu unayopaswa kujiuliza mwenyewe ili kufikia hatua kubwa sana maishani mwako.

Soma Zaidi: Nani Katengeneza Kanuni Hii? Haifanyi Kazi!!

1. Je, ninakwenda wapi?
Unaweza ukawa unatembea lakini ukawa hujui wapi unaenda. unaweza ukawa unakimbia lakini hujui uendapo. Na sio kila akimbiaye anajua aelekeako. Sasa naomba ukae, ujiulize ni wapi huko unaenda?
Swali hili tukiliweka kwa lugha nyingine tutasema,  unayapeleka wapi maisha yako?
Usikurupuke kujibu swali hili hapa. Kaa chini, ujihoji na kuja na majibu makini sana. Ambayo utayaandika chini  na kuanza kuyafanyia kazi.

2. Ninakwenda na nani?
Sio kila mtu anafaa kwenda na wewe, sasa jiulize kwenye safari yako hii ambayo wewe unaiendea wewe, utaenda na nani?

3. Kwa nini unaenda huko?
Usiamue kufanya kitu au kutimiza lengo bila ya kuwa na sababu. Unapaswa kuwa na sababu inayokusuma wewe kufika ng’ambo. Unapaswa kuwa na sababu itakayokuamsha kila siku asubuhi na kukufanya uzidi kusonga mbele.

Soma Zaidi: Maswali Matano Ya Kujiuliza Siku Ya Kuzaliwa
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X