Nnavyoiona Miaka Mitano Ijayo Na Jinsi Utakavyoachwa Nyuma


Kwanza kabisa nashukuru sana uwepo wa elimu hii ambayo tunaendelea kuipata kutoka walimu na watu mbali mbali wanaojitoa kila siku kuhakikisha wanakupa wewe maarifa ya kukutosha. Kwa hakika inatia moyo.

Maarifa yanayotolewa na yanayopatikana kwenye blogu ya SONGA MBELE, yana lengo la kukuelimisha wewe, kukuamusha na kukusaidia ili ufanye makubwa. Lakini kikubwa ni kwamba wewe unapaswa kuchukua hatua kufikia ndoto zako.

Sasa kuna hatari niionayo miaka mitano ijayo.
Kama hutachukua hatua leo hii miaka mitano ijayo kutakuwa na mabadiliko makubwa sana

Miaka mitano kutoka sasa wale wanaochukua hatua na kuwekeza watakuwa kwenye viwango vingine, na hivyo mamilionea wapya watakuwa wameanza kuonekana nchi hii!

Miaka mitano wale unaowaona leo na kuwadharau ila kwa sababu wanapata maarifa sahihi na kuchukua hatua, miaka mitano ijayo wewe kukutana nao itakuchukua mwezi na hata miezi sita kabla hujawaona.
Unawachukulia poa siku ya leo, ila miaka mitano ijayo utapata taabu sana kuonana nao!

Miaka mitano ijayo, waandishi ambao leo hii unaona wa kawaida sana watakuwa waandishi wakubwa sana. Wengi watakuwa wamevuka anga na kwenda kwenye anga za kimataifa! Kwa hakika miaka mitano ijayo kuna makubwa sana yatatokea!

Wapo watu leo hii unawaona wameanza ujasiliamali katika hali ya chini sana, wanafuga kuku, wana duka dogo tu, wanalima mashambani, wameanzisha viwanda vidogo kutaja ila vichache,
Miaka mitano ijayo watu hawa utawakuta kwenye magazeti makubwa ya FORBES, NEWYORK TIMES n.k wakishikilia nafasi za mbele za magazeti kama wajasiliamali machachari sana.

Sima Zaidi: Miaka 20 Iliyopita, Miaka 20 Ijayo

Je, wewe utakuwa umefanya nini miaka mitano ijayo?
Je, wewe utakuwa wapi?

Je, utakuwa umeshasafiri nje ya nchi!
Utakuwa umeandika kitabu?
Utakuwa umewasaidia wengi kufikia ndoto zao?
Utakua umetatua matatizo kadha wa kadha kwenye jamii yako?

Utakuwa umefanya nini?

ANGALIA VIDEO HII: CHUMA HUNOA CHUMA

Miaka mitano ijayo!  Ni miaka inayofurahisha sana, ila kwa watu ambao wapo tayari leo hii kulipa gharama, kuweka juhudi na kuchukua hatua!
Hii ndio miaka mitano ijayo ninavyoiona!

YAJAYO YANAFURAHISHA!!

Upo tayari! Asante sana,
Tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X