TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-011


“Kama mabadiliko pekee unayosheherekea kwenye maisha yako ni sherehe ya kuzaliwa, basi bado hujaanza kuishi”

Rafiki, naomba nikuulize swali, hivi ni lini watu walikaa na kushangilia mafanikio na mabadiliko yaliyokuwa yametokea kwenye maisha yako?

Je, ni siku ile ulipofanya sherehe ya kuzaliwa?

“Kama mabadiliko pekee unayosheherekea kwenye maiaha yako ni sherehe ya kuzaliwa, basi bado hujaanza kuishi”

Kiukweli hatupaswi tu  kuja kwako kila mwaka tunasherehekea sikukuu ya kuzaliwa tunaondoka.
Siku nyingine tutafurahi sana, tukisikia unatuambia umeweza kuvumbua kitu fulani,
Siku nyingine tutapenda kuja kusherehekea uzinduzi wa kitu fulani.

Hata hama hatutafika ila hata ile wewe kufurahi pamoja nami nikiwa mbali kwa sababu umegundua kitu bado na yenyewe inatia moyo?

Swali, hivi yule rafiki yako alipokupost mara mwisho, alikuwa anakusudia kuiambia nini jamii?

Kwamba ni siku ya kuzaliwa?
Au kuna kitu ulifanya ambacho kilimvutia sana kiasi akakupost!!

“kama mabadiliko pekee unayosheherekea kwenye maisha yako ni sherehe ya kuzaliwa, basi bado hujaanza kuishi”

Badilika sasa,
Kuna mabadiliko ambayo tunajua tu kwamba yatatokea kila mwaka.
Kwa mfano kila mwaka tunajua tutauanza na MWAKA MPYA!
Kila mwaka kuna PASAKA
Kila mwaka kuna IDDI
kila mwaka kuna KRISMAS!
Kila mwaka kuna NYERERE DAY!

Na wewe kwako haya ni mabadiliko unayosherehekea tu!? Kwa nini?

Swali la kujiuliza, je, ninataka watu washerekee pamoja nami kitu gani baada ya mwaka, mwezi au wiki?
Tafuta kitu hiki na uhakikishe unakifanyia kazi.

Namalizia kwa kukwambia hivi,
Nimeeleza kwa undani masuala ya mabadiliko kwenye maisha katika kitabu changu kiitwacho JINSI YA KUIBUA UBUNIFU ULIO NDANI YAKO.
kitabu hiki ni 5,000/- tu.
Ukipata nakala tete (soft copy) yako leo, soma kipengele hiki hapa.

Ili upate kitabu hiki, utapaswa kutuma pesa kwanza kwenda nambari 0755848391 jina GODIUS RWEYONGEZA
baada ya hapo nitumie ujumbe wa kunitaarifu pamoja na email yako.
Utapokea kitabu muda mfupi baada tu ya kutuma taarifa yenye barua pepe (email)

Ndimi,
Godius Rweyongeza
www.songambeleblog.blospot.com

Asante sana.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X