Kitabu cha utajiri wa mataifa, kimeandikwa miaka ya 1700. Na ndani ya kipindi hiki suala zima la kuajiriwa lilikuwa linapewa sana kipaumbele. Yaani ajira zilikuwa walau nyingi sana ukilinganisha na leo hii.
sasa leo nimekuwa najiuliza hivi ni kitu gani kikifanya ajira zikapotea? Ilikuwaje miaka hiyo idadi ya watu wanaotafuta ajira ilikuwa ni ndogo ukilinganisha na ajira zenyewe ila sasa ajira ndio hamna kabisa. Swali hili limetawala sana kichwani mwangu siku ya leo. Swali hili limekuja baada ya mimi kusoma sentensi iliyokuwa kama kichokoza mada.
Nimegundua kwamba
👉🏽👉🏽kwa kipindi kile teknolojia ilikuwa bado haijakua na hivyo asilimia kuvwa ya kazi ilikuwa inafanywa na watu wenyewe. Na hivyo kufanya watu wahitajike zaidi.
Ila sasa ukisubiri ajira inakula kwako. Yaani teknolojia imesawazisha kila kitu. Kazi za watu 100 ibafanywa na mashine moja tu.
Kiukweli UTAJIRI WA MATAIFA ukiokuwa unazungumziwa miaka ile na jinsi ulivyojengwa sasa hivi tunaoungelea kwa namna nyingine.
Kwenye kitabu hiki ambacho kimezungumzia historia ya mambo kadha wa kadha kuhusu pesa, ajira, kazi. Kimezungumzia mambo haya yote kwa undani kama yalivyofanyika kipindi kile.
Tunaona mambo ya kuwinda, kilimo, ususi, kufua vyuma n.k
Hii ndio kusema kwamba hatupaswi kuwa wategemezi kwa aina moja ya kujenga uchumi. Mambo yanabadilika.
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA
HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA