UCHAMBUZI WA KITABU CHA WEALTH OF NATIONS-9 (MALIPO KWA WAFANYAKAZI )


Tunaendelea na kitabu che wealth of nations. Kitabu hiki kinazidi kunifungua zaidi na zaidi. Kuna vitu vimekuwa vknaongelewa kwenye zama za sasa kama vile ni vigeni, kumbe vimekuwepo tangu zamani sana.

Ebu, ona mambo haya:
1. Tangu zamani mwajiri anamlipa mwajiriwa kiasi kidogo sana cha pesa kiasi ambacho hakiwezi kumtosha mwajiriwa kukidhi mahitaji yake. Jambo hili linamfanya aendelee kurudi kazini kila kukicha, ili kufanya maisha yake yaendelee.

Maana ni wafanyakazi (waajiriwa) wachache wenye uwezo wa kukidhi mahitaji yao kwa wiki, mwezi na mwaka mzima bila kuhitaji ajira kabisa.

2. Sheria zinamruhusu mwajiri kuwalipa waajiriwa wake kiasi anachowalipa. Na hivyo kuwafanya waajiriwa wawe na njia moja tu ya kuongeza kipato wakiwa kazini. Kufanya kazi kwa bidii ili wapandishwe vyeo.

3. Na kutokana na ukweli kwamba watu wote hawawezi kupandishwa vyeo. Basi watu hudai kupandiahiwa mshahara kama haki zao. Na hivyo waajiriwa huungana na kuamua kudai haki zao ambapo mara nyingi haki hizi wanazidai kwa nguvu, maandamano n.k
Hata hivyo njia hii mara nyingi sana huwa sio suluhisho la ugonjwa wa kipato kidogo.
Kitu ambacho huwa kinatokea ni watu kutulizwa na vyombo vya usalama huku wakiwataka watu warudi kazini ili mwajiri aendelee kuongea na viongozi wao. Jambo ambalo pia huwa halizai matunda yoyote.

Kiukweli kitabu hiki kinaendelea kunifungua zaidi na zaidi.

Usishangae kuona kwamba leo nimeeleza matatizo  zaidi ya suluhisho. Kumbuka kwamba safari bado inaendelea. Kwa hiyo leo nimekudokeza kidogo kuhusu MALIPO KWA WAFANYAKAZI ila kesho tutaendela na mada hii hii  ili tuichambue kwa undani na mwisho wa siku tutapata suluhisho.

Je, upo tayari?

Kama kuna kitu unajifunza, tafadhari sana usisite kuniandikia
Wasap tu 0755848391
Au Email; godiusrweyongeza1@gmail.com

Nami Nitakujibu pia.

Asante sana,
Umekuwa nami,
GODIUS RWEYONGEZA (Songambele)
Tukutane kwenye jukwaa la wanamfanikio.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X