UCHAMBUZI WA KITABU: WEALTH OF NATIONS.-6 (hivi ndivyo bei zilikuwa zinapatikana)


Utajiri Wa Mataifa

Ukurasa wa 50-53

Soma Zaidi;  UCHAMBUZI WA KITABU CHA WEALTH OF NATIONS-5 (Mwanzo Wa Hisa)

Kama mpaka sasa tupo wote, utagundua kwamba uchambuzi wa siku ya jana na leo umetoka kurasa za 50-53
Lengo la mimi kurudia hapa ni kukazia pointi maana hapa nimeona kuna nondo nyingi zimewekwa sehemu moja. Mfano unaweza kuona kutoka kwenye kurasa hizi hapa, jana tuliongelea juu ya mwanzo wa hisa. Na leo kutoka kwenye kurasa hizi hizi  tunazungumzia jinsi bei ya kitu ilivyokuwa inapatikana.

Soma zaidi: UCHAMBUZI WA KITABU CHA WEALTH OF NATIONS-5

Kiukweli naomba ufahamu kwamba kitabu hiki kimezungumzia misingi mingi ya pesa, ilivyoanza, ilivyokua na hivyo kinakupa mwanga wa hapa tulipo na kule tuendako. Mambo mengine yaliyokuwa yakifanyika zamani sana, bado yanafanyika hata leo na mengine yataendelea kufanyika kwa siku zijazo.

Sasa, zamani za mababu wetu ambazo binafsi napenda kuziita ZAMA ZA MAWE. Vitu vilikuwa vina bei kulingana na thamani ya kitu. Japo hawakuwa na pesa lakini mfumo walioutumia kipindi hicho ndio uliruhusu kitu kiwe na bei kiasi fulani.

1. Bei ya kitu ilitegemea muda uliotumika kukipata kile kitu. Kama ilichukua siku mbili kumpata swala wakati huo huo inachukua siku moja kupata sungura basi bei ya swala mmoja ilikuwa ni sawa na sungura wawili.
Kama ilichukua masaa mawili kupata mzizi fulani wakati huo huo inachukua saa moja kuupata mzizi wa aina nyingine, basi bei ya mzizi uliopatikana ndani ya masaa mawili ilikuwa ni mara mbili zaidi ya ule uliopatikana kwa saa moja.

Hiki ni kitu cha kwanza kikichotumika katika kuweka bei.

2. Uwezo na Ujuzi wa mtu.
Kama mtu aliyehusika kupata kitu kile ana uwezo na ujuzi wa hali ya juu, basi bei yake ilikuwa inakuwa kubwa bila kujali muda uliotumika. Hata kama swala angempata ndani ya dakika 10 bado bei yake ilikuwa inapaswa kuwa kubwa maana yeye ni mbobezi kwenye suala zima la kuwinda.

Na ujuzi huu ulikuwa haupatikani haraka haraka kama ambavyo wengi walikuwa wanategemea. Ujuzi huu ulikuwa unapatikana kupitia kufanya kitu mara nyingi kwa kukirudia pamoja na mazoezi.

Jambo kama hili hapa linazidi kujitokeza kwenye zama zetu. Zamu hii halijitokezi kama kwa njia ya kuwinda ila kwa namna nyingine.
Kwa sssa unakuta mtu na utaalamu wake analipwa kiasi kikubwa japo anafanya kazi kwa muda mfupi.
Lakini pia tunaona bei za vitu zinapanda kwa sababu ya uwepo wa mtu fulani. Mfano mtu anaitisha semina ambayo kwa sababu ya uwepo wa mtu fulani basi bei yake inakuwa mara mbili au tatu zaidi. Lakini kama mtu huyo asingekuwepo basi maana yake bei ingekuwa ya kawaida.

Hivi ndivyo bei zilipangwa miaka ya zamani kidogo na mbinu hizi bado zinatumika sasa japo zinaweza kuwa zimeboreshwa zaidi ya hapo nyuma.

Je, wewe bei ya bidhaa zako huwa unaipanga kwa kutumia vigezo gani??

Tafadhali niandikie maoni yako kwenda
Wasapu tu 0755848391
Email: godiusrweyongeza1@gmail.com

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X