utajiri Wa Mataifa
Ukurasa 42-61
1. Mgawanyiko wa kazi unazuiwa na uchache wa soko. Kadri soko linavyokuwa dogo ndivyo watu hufikiria juu ya kufanya kitu kingine kwenye jamii ili kuongeza kipato, na hivyo kuanza kusababisha ushindani. Kwa sababu unakuta mtu anachoenda kufanya kimeshafanywa na mtu mwingine kabla, au anachoanza kufanya baadae kinaigwa na mwingine.
2. Kuna biashara nyingine haziwezi kufanyika vyema kijijini hivyo kulazimika kupelekwa mjini. Hii ni kutokana na ukweli kwamba idadi ya watu kijijini ni ndogo sana.
3. Kama mtu ataamua kufanyia biashara yake kijijini, basi atapaswa kufanya na vitu vingine na vingine ili kuongeza wigo wa kazi zake maana kijijini idadi ya watu ni ndogo sana. Anapoongoza wigo anaongeza idadi ya wateja.
4. Tusikae tu na kuyaangalia mazingira, bali tuwe tayari kuyabadili mazingira kulingana na rasilimali zilizopo. Kama tupo karibu na bahari basi tuangalie jinsi ya kuweza kurahisisha maisha kwa kutumia rasilimali maji.
Kama tupo karibu na nchi kavu basi tuangalie jinsi ya kurahisisha maisha kwa kutumia rasilimali ardhi.
5. Kila mtu ni tajiri au ni masikini kulingana na uwezo wake wa kufurahia, vitu fulani kwenye maisha.
6. Gharama ya kitu, huanza kupimwa kwa kiwango cha kazi na nguvu iliyotumika kukifanya. Kadri nguvu na juhudi inavyokuwa kubwa, ndivyo na gharama yake inakuwa kubwa.
7. Katika sanaa ya kulihudumia soko kuna watu ambao huwa wanafika sokoni kwa muda mfupi, wanauza bidhaa zao na kuondoka. Baada ya hapo wanapotea.
Ila bepari huwa kila wakati anahakikisha bidhaa zake zinakuwa sokoni. Hii humfanya kujenga uaminifu wa hali ya kuu sana kila na hivyo kumfanya avutie wateja kwake zaidi.
8. Kitu kingine ni kwamba bepari hutumia fursa za kuhitajika kwa bidhaa sokoni kuhakikisha anatoa bidhaa bora sana sokoni lakini huitumia nafasi hiyo kuongeza mauzo zaidi ya siku zote.
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA
HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA