Huwezi Kuwa Daudi Bila Jonathan Na Goliati


Hongera sana rafiki yangu kwa kupata nafasi hii ya kipekee sana.
Leo ni ijumaa ya tarehe 23 2018.
Tumebakiza siku 38 kuumaliza mwaka huu. Bado tunao muda wa kukamilisha malengo yetu.

Moja kati ya hadithi ambazo zinapedwa sana na watu kutoka kwenye Biblia ni hadithi ya Daudi na Goliati. Hadithi inatuonesha jinsi mtu mdogo ambaye ni Daudi anampiga MTU mkubwa (GOLIATI) aliyekuwa  akiogopwa na watu.

Kwenye Biblia pia Kuna hadithi ya Daudi na Jonathani. Ambapo Jonathani ni rafiki Wa kweli au rafiki wa damu wa Daudi.

Sasa ili ufanikiwe unahitaji watu wote hawa wawili.
Kwanza unawahitaji akina Jonathani (MARAFIKI WA KWELI). Lakini pia unawahitaji akina Goliati (MAADUI).

MARAFIKI WA KWELI
Sio kila unayeongea naye ni rafiki wako wa kweli. Wapo wengine wanajenga urafiki kwako kwa sababu Kuna jambo ambalo mnapaswa kulifanya kwa pamoja. Jambo hili likiisha huwezi kuwaona tena. Mfano mzuri ni wale uliosoma nao shule ya msingi, sekondari na chuo. Wengi walikuwa MARAFIKI wako kweli. Pengine ulijua urafiki wenu utadumu milele. Ila baada ya kuhitimu Kuna watu hujawahi kuwaona wakikutafuta tena.
Hii ndio kusema kwamba kilichokuwa kinawaunganisha kwa wakati huo, sasa hivi hakipo tena.

Lakini Kuna MARAFIKI hata iweje mpo wote tu. Iwe mpo karibu, mbali. I we mna jambo (mission) mnafanya kwa pamoja au kila MTU anafanya mambo yake, lakini bado mnakuwa mnajihisi mpo pamoja. Hawa ndio akina Jonathani. Ukiwapata MARAFIKI wa aina hii, usiwaache wakaenda zao.

MAADUI/VIKWAZO
Unawahitaji hawa pia ili uweze kufanikiwa. Nakubaliana na mwanamziki mmoja ambaye aliimba, akisema, ili ufanikiwe unahitaji marafiki, lakini ili ufanikiwe zaidi unahitaji maadui. Unaona sasa. Mwanmziki huyu hakuwa mbali na Robert Greene aliyesema, kama hauna maadui, tengeneza maadui ili uweze kufanikiwa, na ufanye nao kazi.

Unapokuwa na maadui watakupinga, watakucheka, watakudharau. Sasa kazi yako itakuwa kufanya vizuri zaidi ya wao wanavyofikiri.
Ukishinda maadui au vikwazo unakuwa umekua zaidi.
Namalizia hapa kuangalia maneno ya Grant Cardone, ambaye anasema, ili awe Raisi wa marekani basi anahitaji nusu ya wamarekani imchukie😀😀

Kama huelewi jinsi ya kuwatumianl maadui wako kwa manufaa, usikurupuke. Tafadhali wasiliana nami, nikupe njia sahihi za wewe kuweza kufaidika nao. Au soma Kitabu cha 1. ROBERT GREENE, (48 LAWS OF POWER)
2. GRANT CARDONE, BE OBSESSED OR BE AVERAGE
3. HOW TO WIN FRIENDS AND INFLUENVE PEOOLE
4. DAVID AMD GOLIATH cha Malcolm Gladwell


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X