Kama Pesa Haiwezi Kununua Kitu Hiki, Umasikini Utaweza??


Kumekuwepo na semi mbali mbali zinasemwa juu ya pesa. Wengine wanasema, pesa sio kila kitu. Wengine wanasema  pesa ni chanzo cha maovu yote, (japo Biblia inasema, upendo wa pesa ni chanzo cha maovu)

Soma Zaidi; Aliyeandika Pesa Ni Chanzo Cha Maovu Yote, Hakuwa Na Senti Haya Moja

Ukiingia google utakutana na makala zenye vichwa kama hivi hapa

1. Mambo 25 ambayo pesa haiwezi kununua
2. Vitu 23 ambavyo pesa haiwezi kununua
3. Vitu 50 ambavyo pesa haiwezi kununua.
Na makala nyingine nyingi sana zinazozungumzia vitu ambavyo pesa haiwezi kununua.baadhi ya vitu hivi ni
Furaha
Upendo
Kusudi la maisha
Tabia
Urafiki
Heshima
  Kujitambua
Amani ya Ndani n.k

Soma Zaidi: Je,Kupenda Pesa Ni Chanzo Cha Maovu?
Orodha ni kubwa sana, kama unaipenda ingia Google sasa ujionee mwenyewe.
Kwa sasa hivyo vinatosha.

Lakini swali langu kama pesa haiwezi kununua vitu hivi, umasikini unaweza? Je, umasikini unaweza kununua furaha, je, ukosefu Wa pesa unaweza kununua upendo?
Jibu ni HAPANA. Tena hapana kubwa. Afadhali kuwa na pesa kunaweza kusaidia kuimarisha vitu hivi lakini sio umasikini. Kwa hiyo basi Leo nataka ujue sehemu ulipo ukomo Wa Kila kitu.
Jua kwamba Unapaswa kuwa na pesa, lakini pia Unapaswa kujua namna ya kuwa na furaha, kuimarisha mahusiano na urafiki.

Lakini sio kuwa masikini.  Namna nzuri ya kuishi maisha bora ni kuwa na pesa, japo pesa sio Kila kitu. Lakini pesa ni muhimu sana.

Ukitaka kujua umuhimu Wa pesa ishiwa kabisa, yaani usiwe na senti wakati huo huo ukutane na mazingira yanayohitaji pesa. Hapo ndipo utajua umuhimu wa pesa kabisaaa! Asante sana, tukutane kwenye meza ya wanamafanikio

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X