Siku moja ina masaa 24. Yakipita ndio yamepita, yaani hayarudi tena. Ndani ya masaa haya kuna vitu vingi sana unaweza kufanya. Ila kama unataka kuongeza ufanisi kazini hupaswi kufanya vitu vyote hivyo.
Ufanisi hautokani na idadi kubwa ya kazi ulizonazo. Ufanisi unatoka kwenye kazi kidogo ambazo unaweza kuzifanya kwa viwango (ubora) vya hali ya juu sana.
Hivyo kila siku, hakikisha unafanya kazi kwa ufanisi mkubwa sana zaidi ya jana.
Kuna njia nyingi sana za kukufanya uweze kuongeza ufanisi katika kazi ambazo unafanya. Na njia hii ni kupangilia mambo makubwa matatu ya kufanya ndani ya siku husika.
Usishangae wala usihangaike, eti kwa sababu una mambo mengi sana, jiulize, hivi kati ya haya mengi, kama ninapaswa kukamilisha kazi tatu tu, ni zipi kazi hizi tatu nitapaswa kukamilisha?
Tafuta kazi ambazo ni za muhimu sana tatu na zifanye.
Fanya hivi Kila siku. Yaani Kila iitwayo leo, pangilia kazi kuu tatu za kufanya ambazo utatumia muda wako, nguvu na akili. Kwa kufanya hivi utakuwa umejiweka katika nafasi nzuri ya kufanya kazi chache ila kwa umakini Wa hali ya juu sana.
Ngoja nikwambie kitu, kati ya watu 10 utakaokutana nao, ni wachache sana ambao wao, wanajua vitu vitatu vya kufanya ndani ya siku yao. Yaani wachache sana. Idadi inaweza isizidi 2.
Ukishakuwa na vitu vitatu, hapo unaweza kuongezea vitatu vya ziada vidogo. Na kufanya orodha yako kuwa na vitu sita.
Sasa pangilia jinsi ambavyo utafanya na kukamilisha vitu hivi. Jiulize ni kipi kianze, kipi kifuate, na kipi kiwe cha mwisho.
Naomba nikukukumbushe kitu kimoja. Hauna muda wa kukutosha kukimbizana na kila kitu. Ila una muda wa kufanya, kazi zako za muhimu sana kila leo. Hivyo weka nguvu yako katika kufanya kazi hizi chache ila zenye umuhimu mkubwa sana.
Sasa kazi ya kufanya baada ya hapa.
Andika vitu vitatu ambavyo utafanya siku hii ya leo.
Ongeza vitatu vya ziada.
Sasa kavifanyie kazi vitu hivi!
Asante sana, tukutane kwenye jukwaa la wanamfanikio
Soma Zaidi; KONA YA SONGAMBELE: Jinsi Ya Kuongeza Ufanisi Kazini-3
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA
HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA