Huu Ndio Uwezo Mkubwa Sana Ambao Unao Ndani Yako


Hongera sana rafiki kwa zawadi ya siku hii njema sana. Leo ni siku yetu ya kipekee sana hakikisha unaitumia vyema sana.

UCHAMBUZI WA KITABU CHA WEALTH OF NATION-9 Malipo Kwa Wafanyakazi

Siku ya leo napenda nikwambie uwezo wa kipekee sana mbao umejilaza ndani yako.
Hivi umewahi kujiuliza kwamba una uwezo gani wa kipekee ndani yako?
Je, ni kuongea?
Je, ni kuchamhua mambo?
Je, ni kudadisi vitu?
Au kuandika! Au kufanya magumu yawe rahisi??

Kwa namna yoyote ile, katika hali yoyote ile. Una uwezo mkubwa sana kuliko ambavyo unafikiri.
Na uwezo huu ni wa kufanya vitu katika viwango vya kuwashangaza watu.

Neno kushangaza, najua utakuwa umelitumia Mara nyingi sana katika lugha ya kigeni ya kiingereza ambapo huku linajukikana kama TO ASTONISH. Neno hili asili yake kabisa ni kilatini. Ambapo walatini hulitamka na kuliandika hivi “EXTONARE”, maana yake, kuwaacha watu wakiwa wamepigwa na radi. Sasa hapa ndipo pa kushangaza zaidi. Yaani, una uwezo Wa kufanya vitu kwa ubora kiasi kwamba  watu wakiona kazi zako basi ule mshangao wao unakuwa sio wa kawaida. Yaani wanashangaa! Na kushangaa na kushangaa!!

Na uwezo huu unaweza kuutumia popote pale, iwe ni kwenye sanaa, sayansi, uchoraji, uchongaji, BIASHARA, uandishi, michezo, n.k
Tafuta eneo moja sasa na ulifanyie kazi.

Asante sana,
Utumie uwezo huu.
Tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X