IJUE NGUVU YA KIDEO NA UNAVYOWEZA KUITUMIA KUONGEZA MAUZO


Kuna njia mbali mbali unaweza kuzitumia kutangaza bidhaa zako na kuongeza mauzo.
Kwa Leo napenda uijue nguvu ya kideo hasa kwenye zama hizi za taarifa, ambapo kila kitu kipo kiganjani! Yaani, kila taarifa unayo mkononi.

Video ni njia ambayo unaweza kuitumia kutangaza bidhaa, kujitangaza au kuonesha kile ulichonacho.
Zama za sasa hivi, zimehamia mtandaoni. Yaani kila kitu sasa hivi, kipo kiganjani.

Kwa hiyo ukitaka kuuza zaidi sasa hivi, tengeneza video moja nzuri inayovutia na isiyochosha. Baada ya hapo itume kwenye mitandao ya kijamii. Utashangaa kuona video hii inasambaa sana mitandaoni na kuwafikia watu ambao hujawahi kukutana nao.

Wakati unatengeneza video yako, naomba udhibitishe yafuatayo.
Biashara yako ni IPI?
Inashughulika na nini?
Insaidiaje mtu anayeiona Mara ya kwanza,
Kwa nini biashara yako iwe ya kutegemewa kuliko kitu kingine.

Lakini pia kama watu wanakujua unaweza kurekodi kideo unapopokea mzigo mpya kwenye BIASHARA yako. Hii itawafanya watu wapende kuwa Wa kwanza kuja kununua bidhaa kwako.

Rekodi kideo unapotuma bidhaa kwa watu wengine. Hii itaonesha uaminifu wako na kwa nini watu wanapaswa kukutegemea wewe.

Rekodi kideo unapokuwa na mtu ambaye ametumia bidhaa zako na zimemsaidia.

Rekodi pale ukikutana na mtu ambaye umekuwa ukifanya BIASHARA naye kwa muda, na yeye awahimize wengine Kuna kufanya na wewe.

Kideo ni njia nzuri, Ila sio njia ya kufanya Mara moja. Fanya Mara nyingi sana kadri uwezavyo.
Rekodi na kutuma kideo kimoja walau kila wiki. Kwa jinsi hii utawafanya watu wakuzoee na watapenda kuja kufanya BIASHARA na wewe

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X