Kuna kitu Nataka kuandika hapa! Kuna kitu Nataka kuandika!


Kuna kitu Nataka kuandika hapa! Kuna kitu Nataka kuandika!

Siandiki kwa sababu ya huyo anayeonekana anaanguka ila Kuna kitu Nataka kuandika hapa! Ndio nataka niandike kitu!

Kwanza najua video hii umeiona mara nyingi sana kabla ya hapa. Lakini sasa nataka uiangalie kwa namna ya tofauti. Ninataka uone kile ambacho ulikuwa hujakiona. Ndio maana nakwambia Kuna kitu nataka kuandika hapa.

Kwanza kabisa naomba wewe uniambie umeona nini? Je, kwa nini umefikiri hivyo?
Sasa hapa Kuna mambo saba ambayo ulikuwa hujayaona kwenye video hii, haya hapa:

1. UNAPOFANYA KITU, KIFANYE KWA JUHUDI.
Najua neno kujituma sio geni kwako, lakini je uwa unalitumia. Ebu rudi hapo kwenye video uangalie hiyo video vizuri. Utagundua kwamba Diamond aliweka juhudi katika kitu alichokuwa anakifanya kwa *kumaanisha na kwa juhudi kubwa*.
Sasa je, wewe unafanya hivyo? Bado kuna kitu nataka kuongea

2. UNAPOJITOA JITOE KWELI
Ukiamua kufanya kitu, kifanye kweli! Hivi hiyo video umeiona vizuri? Naomba urudi uiangalie tena! Yaani sio ya mtu anayefanya utani!
Diamond ameanguka chini lakini bado anatoa Sauti kuendelea kutumbuiza watu wanaomsikiliza.

Sasa wewe ukijikwaa tu ndio basi hutaki kuendelea! Ebu acha utani aisee! Bado kuna kitu nataka kuandika hapa!

3. UKIWEKA JUHUDI LEO, MALIPO YAKE UTAYAPATA KESHO.
Naomba nikuulize kitu! Hivi wewe kwa kitu unachokifanya, Leo hii ukitaka watu wanaofuatilia kazi yako waje watakuwa wangapi?
Najaribu kufikiria kama wewe ni mpiga umbea, ukiitisha tamasha la umbea leo hii watafika wangapi kushuhudia unavyopiga umbea?
Au kama wewe ni mlevi ukiitisha tamasha la ulevi Leo hii watafika wangapi kukuona unavyolewa!!
๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€

Sasa rudi ukaangalie hiyo video. Niambie unaona watu wangapi waliohudhuria kwenye hilo tamasha?
Ndio maana nakwambia. Ukiweka juhudi leo, kesho itakulipa.
Kwa hiyo weka juhudi katika kile ukifanyacho, weka juhudi na weka juhudi tena. Nina hakika ukimuuliza Diamond mambo yalivyokuwa siku ya kwanza anaanza mziki na leo hii atakwambia hadithi mbili tofauti!
Bado Kuna kitu nataka kuongea hapa! Ndio kuna kitu nataka kuandika hapa hapa!


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X