Tafadhali Usimkumbatie Mtu Huyu, Atakuumiza Sana


Hongera sana kwa siku hii njema sana. Leo hii ni tararhe 09 Disemba. Zikiwa zimebaki siku 22 mwaka wetu ufike ukingoni.

Kwa kawaida watu tumekuwa na utaratibu Wa kukumbatiana hasa pale tunapokutana na watu. Kukumbatia imekuwa ni ishara ya kukaribishwa kwa mtu, upendo na furaha anayoionesha mtu kwako. Ukitaka kujua kwamba mtu amekukaribisha, basi ishara moja wapo ni kunyoosha mikono take Mbele kama inavyofanyika wakati Wa kukumbatia. Hata hivyo ukiona mtu ameweka mikono yake nyuma jua kwa wakati huo asingependa uwe karibu yake. Na wala usimsogelee.

Sasa wewe pia kwenye maisha Kuna watu Unaopaswa kunyoosha mikono mbele kuwapokea na Kuna watu Unaopaswa kunyoosha mikono Nyuma, ili wasisogee karibu yako. Na watu hawa ambao hupaswi kunyoosha mikono kwao ni
1. Watu wanaokukatisha tamaa. Ukiona mtu anakukatisha tamaa, ukiona unafanya hiki yeye haoni umuhimu wake. Unatimiza ndoto zako yeye anakuvuta ili uachane nazo. Basi wewe achana naye kabla hajasababisha madhara kwako

2. Watu wanaosema maneno hasi.
Kuna watu wao Kila wakati maneno yao ni kukurudisha Nyuma. Utasikia wanasema, achana na hicho. Usiende huko. Huwezi hiki. Utaweza kama nani na maneno mengine mengi. Watu Wa namna hii sio wa kuambatana nao.

Waache waende kivyao na wewe chagua njia nyingine ili uweze kuandika jina lako kwenye dunia hii. Asante sana rafiki yangu na kuwa na siku njema sana

Soma Zaidi; Huu Ni Aina Ya Ubabe Unaopaswa Kuuonesha

Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA
Hakikisha umesubscribe kwenye YouTube Channel Yangu Ya Youtube Kwa Kubonyeza Hapa


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X