TAFAKARI YA WIKI: Kuna watu wana shahada na wengine wana cheti cha shahada.


Siku moja profesa aliwapa wanafunzi wake kazi ya kufanya. Ili kazi hiyo iweze kufanyika vizuri, na kwa weredi wa hali ya juu sana basi aliwagawa wanafunzi wake katika makundi. Lengo la profesa huyo lilikuwa ni kuwaleta wanafunzi wake pamoja, ili washirikishane ujuzi, wajadiliane na kuja na kitu kimoja kikubwa.

Kazi iliyotolewa na profesa kwa  wanafunzi wake ilikuwa ni kuzunguka maeneo mbalimbali na kukusanya taarifa mbalimbali za mbolea za viwandani, zinazopatikana katika mkoa mmoja hapa nchini.

Kama ilivyo kawaida wanachuo wakishajua kwamba kazi ni ya kundi kila mmoja anaanza kumtegea mwenzake. Kila mmoja anasubiri mwenzake afanye ili mwisho wa siku na yeye jina lake liandikwe kwenye kazi ile na yeye aonekane kama mshiriki.

Sasa katika kundi mojawapo, wanafunzi wote walikaa kimya wala hakuna aliyekuwa tayari kusema tufanye kazi. Siku za kufanya kazi zilizidi kuyoyoma huku kila mwanafunzi akizidi kumkwepa mwenzake. Kila mmoja alikuwa anasema fulani.

Kwenye kundi hilo kulikuwa na mwanafunzi anayeitwa Rose. Aliamua kujitolea kupanga siku ya kufanya kazi. Aliwapa wanafunzi wenzake, taarifa ili wakutane kufanya kazi. Ila cha kushangaza siku ya kazi hawakutokea. Wanafunzi waliopaswa kutokea walikuwa 11, waliofika eneo la tukio ni wanne. Kati ya hao wanne wawili wakifika tu ilimradi waonekane. Baada ya kufika walianza kusingizia kuchoka, mtihani na mambo mengine.

Kwa hiyo Rose alijitolea kuifanya kazi huku akijua kwamba mwisho wa siku  kazi itahesabika kama kazi ya kundi zima. Yaani hata wale ambao hawakushiriki kazi nao watahesabika kama waliofanya kazi. Ndipo Rose alikuja kugundua kwamba chuoni, kuna watu wanasoma na kupata shahada, ila kuna watu wanapata vyeti vya shahada.

Kadri ya Rose tofauti ya watu hawa ilikuwa ni
👉👉wanaopata cheti ni wale ambao wanahitimu chuo kwa kuwa na cheti ila hawana maarifa yanayoendana na cheti.

👉👉Kadri ya Rose, unaweza kusoma chuo mwaka mmoja, miwili mitatu na kuendelea ila mwisho wa siku ukawa hujapata  shahada ila umepata cheti.

👉👉ukipata cheti unakuwa huna ujuzi na uelewa unaoendana na cheti hicho. Ndio maana Rose anawaita wenye cheti. Sasa je, wewe una cheti au una shahada?

👉👉Mwenye cheti, mara baada ya kuhitimu haongezi maarifa zaidi, anasema kwamba nilishasoma tangu zamani sana

Tafakari! Chukua hatua.

Soma Zaidi; TAFAKARI YA WIKI; Elimu Ya Chuo Haitoshi, Kitu Kimoja Unachopaswa kuambatanisha Na Elimu Ya Chuo

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X