Ukiona unafanya kitu ila haukifanyi kwa namna ya kueleweka. Ukiona unafanya kitu ila ukahisi kama bado unakosa kitu fulani hivi, basi hapo unapaswa kujua kwamba hauna maarifa ya kutosha.
Usikimbie kitu hicho kwa sababu hujaweza kukifanya vizuri. Badala yake kimbilia kutafuta maarifa zaidi na zaidi ili uweze kukifanya kwa ubora.
Moja kati ya watu wa namna hii walikuwa ni Thomas Edison. Katika kazi kushindwa kwake mara elfu kumi hakuacha. Bali kila mara alitafuta maarifa mapya ambayo hakuwa nayo ili aweze kufanya kitu kwa ubora zaidi.
Sasa kabla ya wewe kuacha jiulize mimi ni nani kuacha? Badala yake kaa kwenye meza na jifunze kisha endelea kufanya ili uweze kufanya kwa ubora zaidi.
Asante sana,
Tukutane kwenye jukwaa la wanamfanikio
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA
HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA