Hii Ndio Aina Ya Maarifa Unayopaswa Kuyapata


Hongera sana rafiki yangu kwa siku hii ya kipekee sana.
Kama umesahau ni kwamba zimepita siku 19 tangu mwaka huu uanze. Sasa karibu sana kwenye somo la leo.

Watu huwa wanaanzisha vitu ila huwa havidumu. Kuna watu huwa wanaanza kusoma  ila mwisho wa siku hawamalizi kozi wanazozianza.
Kuna watu huwa wnajiunga na mafunzo fulani mtandaoni ila mwisho wa siku wanaacha.

Sasa hii sio njia nzuri ya kujifunza katika maisha yako. Kama umekuwa na tabia hii, napenda nikwambie kwamba achana nayo mara moja. Itakupoteza sana.

Sifa kuu ya maarifa Unayopaswa kuyapata ni kwamba upate MAARIFA YALIYOKAMILIKA.

Hii ndio kusema kwamba ukianza kusoma Kitabu kisome mpaka mwisho.
Sio tu unakimbilia kwa sababu ya kuona kichwa cha kitabu na kuishia njiani.
Ukianza kusoma kozi iwe ni chuoni au mtandaoni, hakikisha unaenda nayo mpaka mwisho.
Ukianza kujifunza kwa mwalimu fulani hakikisha unapata maarifa yake mpaka mwisho.

Sifa ya maarifa ni kwamba yakamilike.

Ukiwa na maarifa nusu, utafanya maamuzi nusu na kuchukua hatua nusu, mwisho wa siku matokeo yatakuwa mabaya.

Maarifa ni kama kanuni. Katika hesabu ukijifunza kanuni au ukiiandika ikiwa nusu. Usitegemee kupata jibu sahihi. Siku zote jibu sahihi hupatikana kwa kutumia kanuni sahihi.

Maarifa sahihi na yaliyokamilika. Hukupa matokeo yaliyokamilika.

Asante sana,
Tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio.

Soma Zaidi; Vitu Viwili Vitakavyotokea Endapo Utakaa Usipopaswa Kuwa

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


2 responses to “Hii Ndio Aina Ya Maarifa Unayopaswa Kuyapata”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X