Hili Ni Jambo Litakalokupa Uhuru Maishani Mwako


Uhuru! Uhuru! Uhuru!

Miaka mingi sana Tanzania ilipata uhuru kutoka kwa wakoloni. Mara tu baada ya uhuru mwalimu Nyerere alikuwa na haya kusema.

Watanzania tunapaswa kupambana na maadui wakuu watatu ambao ni ujinga umasikini na maradhi.
Vitu hivi vitatu mwalimu aliviita maadui wa taifa.

Ila dawa ya vitu hivyo vyote vitatu ilikuwa ni elimu.
Ujinga ni matokeo ya kutokuwa na elimu.
Maradhi pia ni matokeo ya kutokuwa na elimu.
Umasikini pia ni matokeo ya kutokuwa na elimu.

Kwa hiyo dawa ya vitu hivi vyote ni elimu, elimu, elimu.

Hii ndio kusema uhuru wowote haukamiliki kama mtu hauna elimu. Wala hakuna uhuru bila elimu.

Kwa hiyo jitahidi sana kuwekeza katika elimu.
Kwa mfano umasikini wako wa sasa hivi  ni matokeo ya kutokuwa na elimu. Anza kuwekeza katika kujifunza ili uweze kuwa na elimu zaidi itakayikufanya usongembele mwaka huu.
Unahitaji elimu ya fedha ili uondokane na umasikini. Hapa hakuna utani, ukiwa na elimu utajenga maisha ya tofauti.

Pata elimu kwa kusoma vitabu
Pata elimu kwa kuhudhuria semina
pata elimu kwa kusikiliza watu wanachosema.

Soma Zaidi; Ndoto Haziwi Ukweli Ukiwa Umelala

Kheri Ya Mwaka Mpya Na Mambo 12 Unayopaswa Kufanya Kuanzia Leo
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X