Ninajua kwamba kila siku unakuwa na majukumu mengi sana ya kutimiza. Kuanzia majukumu ya kazi, biashara, familia na mengine mengi. Kati ya hayo majukumu huwa unajikuta huyatimizi kila siku.
Sio kwamba huyatimizi kwa sababu ya ukubwa wake. Bali huyatimizi kwa sababu ya hujajua kitu hiki kimoja.
Na kitu chenyewe ni kwamba MAJUKUMU MADOGO NDIO HUWA YANAWASHINDA WATU KUYATIMIZA.
Vitu vunapoonekana rahisi sana, inakuwa rahisi kwako kuvighairisha. Unajisemea utafanya baadae au kesho, na hivyo kujikuta siku imepita, kesho yake pia imepita.
Ila sasa upande wa pili kitu cha kushangaza ni kwamba majukumu madogo ndio huleta mwisho wa siku huleta matokeo makubwa sana yakiunganishwa.
Sasa leo nakupa dawa ya kuwa unatimiza majukumu yako madogo madogo kila siku. Na dawa hii sio nyingine bali mi kupanga ratiba kila siku na kuhakikisha unayatimiza, basi. Hakuna siri zaidi ya hapo.
Soma Zaidi; Vitu Vitano Vinavyoharibu Ubunifu Wa Tanzania
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA