Bila shaka umewahi kusikia usemi unaosema kwamba hesabu baraka zako! Usemi huu unapenda tuwe watu wa kushukuru nakuona mazuri pale ambapo wengine wanaona mabaya. Kiukweli kuna mambo mengi sana ambayo unaweza kushukuru Kila iitwayo leo. Ni mengi sana ndio maana unapaswa kuhesabu baraka zako.
Ebu ona hapa;
1. Leo hii bado unavuta pumzi na kuishi wakati kuna watu wengi sana ambao tayari wamepoteza uhai. Sasa kwa nini usihesabu baraka zako!!
Kuhusu hili kuna mtu mmoja ambaye kila alipokuwa anakutana na mgeni au rafiki yake alikuwa anafurahi sana. Sasa siku moja akaulizwa, hivi kwa nini huwa unafurahi sana ukikutana na mtu. Alikuwa na haya ya kusema
Katika maisha yangu nimeona wafu wengi. Hivyo nikikutana na wewe upo hai lazima nifurahi sana.
Jambo hili linatuelekeza kwenye pointi yetu ya pili siku ya leo ambayo inasema hivi,
2. Hesabu baraka zako ukikutana na mtu.
Kiukweli ni baraka sana wewe kukitana na rafiki fulani au mtu fulani muda fulani. Yaani, ni baraka sana. Mtu huyo angeweza kuwa amekutana na mwingine lakini amekutana na wewe. Sasa kwa nini usihesabu baraka.
3. Hesabu baraka zako unapogundua kilichokuleta duniani.
Hapa ndipo patamu sana, maana yake utaenda kuwasaidia watu wengi kuishi maisha bora sana. Hesabu baraka kwamba umekuwa wewe.
4. Hesabu baraka zako pale unapopata hata mtu mmoja Wa kukubali kile unachofanya, hata kama mtu huyu ni mzazi wako pekee anayekubali unachofanya. Hii ni baraka kubwa sana.
Kuna maeneo mengi sana ambapo Unapaswa kuhesabu baraka zako. Ebu anza leo kuhesabu baraka hizi.
Soma Zaidi: Haya Ni Mambo Manne (04) Ambayo Unapaswa Kuyafanya Asubuhi
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA