Kheri Ya Mwaka Mpya Na Mambo 12 Unayopaswa Kufanya Kuanzia Leo


Kheri ya mwaka mpya rafiki yangu, leo ni tarehe mosi januari 2019. Hongera sana kwa nafasi hii ya kipekee sana ya kuuanza mwaka huu.

Najua hii ndio siku uliyokuwa umeisubiria kwa siku nyingi sana, sasa hakikisha kwamba unaitumia vyema kabisa. Mwaka huu ni mwaka wako, utumie vyema ili uzidi kusonga mbele. Huu ni mwaka wako wa mafanikio makubwa sana, kiukweli utumie ili kufikia mafanikio makubwa zaidi.

Sasa kuna mambo 12 ambayo Unapaswa kuyazingatia tangu mwaka huu unaanza mpaka utakapoufikisha mwisho mwaka huu.

1. Usiishie tu kuangalia watu wanasababisha matokeo mwaka huu sababisha matokeo.  Kwa lugha nyepesi niseme hivi, mwaka huu usiwe shabiki kuwa mchezaji.

2. Anzia hapo ulipo kufanya kinachowezekana ili uweze kufikia yasiyowezekana ndani ya mwaka huu. Kama una malengo makubwa anza kuyafanya kwa udogo, kwa kutumia RASILIMALI ulizonazo sasa.

3. Usisubiri fursa mpya. Wala usisubiri watu wakutengenezee fursa mpya 2019! Wewe  tengeneza fursa mpya Ndani ya mwaka huu.

4. Ukiogopa kuchukua hatua mwaka huu, usitegemee matokeo makubwa. Matokeo makubwa ni matokeo ya kuondokana na uoga.  Kama kuna muda wa kuachana na uoga basi mwaka huu ndio mwaka sahihi. Kwani uoga umekusaidia nini mwaka jana?
Kwani uoga umekusogeza wapi mwaka jana?
Ebu kwa siku 365 zijazo weka uoga pembeni na pambana kufikia malengo yako.

5. Mwaka huu ni mwaka wa kubadili hasi kuwa chanya. Mwaka wa kutengeneza juisi kutoka kwenye limau, mwaka wa kubadili matatizo kuwa fursa. Hakikisha unautumia vyema.

6. Watu wakisema huwezi, wewe waoneshe kuwa umeweza. Hakuna kitu huwa kinaumiza watu kama kuona kwamba umeweza kile walichosema hakiwezekani.

Kwa hiyo mwaka huu badala ya kubishana na watu kwamba unaweza. Waoneshe watu kwamba umeweza.

7. Fanya uwekezaji Ndani ya mwaka huu mpya. Hakuna kitu kinadumu muda mrefu sana kama uwekezaji. Na uwekezaji nambari moja wa kufanya mwaka huu ni kuwekeza katika maarifa. Wekeza katika kutafuta ujuzi, elimu na kusoma vitabu zaidi mwaka huu.

8. Ukikutana na mzigo/kikwazo/tatizo basi jua kwamba una mabega ya kupambana nacho. Hakuna kitu kilichombele yako ambacho wewe huwezi kupambama nacho.

9. Huhitaji kuwa na jina ili uanze, ila unahitaji kuanza ili kujenga jina lako.

10. Mafanikio makubwa mwishoni Mwa mwaka Ni mjumuiko wa vitu vidogo vidogo unavyofanya Kila siku kuanzia januari mosi

11. Ili uweze kuwa bora lazima uwe tayari kupambana na changamoto, vikwazo na matatizo. Juu ya hili Tonny Robins aliwahi kusema, ni matatizo yanayotufanya tukue bila matatizo tusingekua.

12. Siku zote amini kwamba mambo makubwa sana yapo njiani kutokea. Kwa hiyo mwaka huu mzima amini mazuri yatatokea mbele yako na kweli mazuri yatakutokea.

Soma Zaidi; Naam! Kipenga Kimepulizwa 2018

Asante sana
#kipengakimepulizwa2019

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X