Kitu Hiki Huwezi Kukiepuka Mwaka Huu


Hongera sana rafiki yangu kwa siku hii njema sana. kwa hakika leo ni siku ya kipekee sana ambayo wewe unapawa kuhakikisha kwamba unaitumia vyema sana ili uweze kusonga mbele na kujikuta kwamba unafanya mambo makubwa.
Kwa kawaida kuna vitu ambavyo huwa unaambiwa kwamba uviepuke ilil uweze kuwa na maisha ya namna fulani. Au kabisa unaambiwa kwamba unapaswa kufuata kanuni fulani ili uweze kuwa na maisha mazuri sana. kwa mfano ili kuepuka ugonjwa fulani basi unapaswa kuhakikisha kwamba unafuata kanuni fulani na unapaswa kuepuka vitu fulani. Na kweli ukifuata kanuni au kuepuka vitu fulani hivyo unakuwa kwenye njia ya wewe kusonga mbele na kufikia mafanikio makubwa sana katika kilekitu ambacho wamekwambia kwamba ufuate au achane na kitu husika.
Sasa kuna vitu ni vigumu sana kuviepuka. Hata iweje, kuna vitu ambavyo lazima utakutana navyo tu.  Na kwa mfano mwaka huu mizima mpaka unafika mwishoni kuna kitu ambacho utapaswa kuendana nacho mpaka mwisho. Kabisaaa hutaweza kukiepuka. Na kitu hiki sio kingine bali mabadiliko. Hakuna jinsi ambavyo utaweza kuepuka mabadiliko ndani ya mwaka huu mpya wa 2018. Mwaka huu mabadiliko lazima yatatokea na hivyo kuwa tayari uyatumia kwa manufaa yako. lakini pia na wewe kuwa chanzo cha mabadiliko haya.

Soma Zaidi: IJUE KANUNI YA UJENZI WA GHOROFA NA HAKIKISHA UNAITUMIA

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X