Zawadi nne(04) Kubwa Inazoweza kujipatia 2019


Tumezoe kwamba huwa tunanunua zawadi kwa ajili ya rafiki zetu, ndugu jamaa na marafiki.
Na pengine huwa kuna misimu ambapo watu hujikita zaidi katika kununua zawadi. Watu huiita misimu hii kwamba ni misimu ya zawadi.
Misimu hii inaweza kuwa ni ya sikukuu au siku ya wapendanao, siku ya mama au baba n.k

Katika kipindi hiki huwa tunawanunulia wengine zawadi ila sisi wenyewe huwa tunajisahau. Sasa mwaka huu usijisahau. Kuna zawadi muhimu zimewekwa kwa ajili yako na unapaswa kuzipata wewe tu! Je, unajua zawadi hizi ni zipi?
Zawadi hizi ni
1. Kulala mapema na kuamka mapema
Mwaka huu jipe zawadi. Sifa kuu ya zawadi hii alizitoa Benjamin Franklin mmoja wa waanzilishi wa taifa la Marekani.  Alisema, “kulala mapema na kuamka mapema, kunamfanya mtu mwenye afya, tajiri na mwenye busara”

Huwezi kuamka mapema kama hulali mapema. Na ukiamka mapema maana yake utapata nafasi ya kufanyia kazi afya zako tatu. Afya ya mwili (utapata kufanya mazoezi kwa dakika kadhaa)
Afya ya akili, (utapata kusoma Kitabu)
Afya ya roho, (utapata kusali)

Lakini pia akili yako ikiwa sawa na afya njema maana utajiri utakuwa unakunyemelea. Mwisho wa siku utajikuta umekuwa tajiri.

Na kwa kuwa unapata maarifa sahihi, basi busara zitakufuata.

2. Kuwekeza katika maarifa
Mwaka huu jipe zawadi ya kutafuta maarifa kwa nguvu zako zote. Soma Vitabu ambavyo rafiki zako hawasomi. Kwa jinsi hii utapata maarifa ya kukutofautisha!

3. Kuthubutu (kuweka maarifa katika matendo)
Ukishapata maarifa basi yaweke katika matendo. Usiishie tu kujua au kusoma kitu. Kiweke katika matendo

4. Kusonga mbele bila kuishia njiani.
Zawadi ya mwisho ambayo utapaswa kujipa mwaka huu ni kuhakikisha unapoanza kitu hauishii njiani. Songambele mpaka kieleweke.

Soma Zaidi; Vitu Viwili Vitakavyotokea Endapo Utakaa Usipopaswa Kuwa

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X