Hapa Ndipo Mabadiliko Makubwa Huanzia


Maisha yanahusisha mabadiliko mengi sana. Kuna mabadiliko ya vipindi vya mwaka. Kuna mabadiliko ya hali ya hewa. Kuna mabadiliko kati ya siku moja na nyjngine. Kuna mabadiliko kutoka sehemu moja kwenda nyngine.
Kuna mabadiliko kati ya mwaka mmoja na unaofiata.

Mabadiliko haya hutufanya tukae tukijua kwamba hatupaswi kutulia na kitu kimoja au kuridhika na hali ile ile Kila iitwayo Leo. Bali na sisi tunapaswa kubadilika kadri ya mabadiliko. Au pengine sisi tusababishe mabadiliko.

Na hapa ndipo pazuri, maana mabadiliko aliyosababiaha binadamu ni ya muhimu sana. Mabadiliko haya ndiyo humwinua MTU na kumfanya azidi kusonga Mbele.

Wewe, ukiwa miongoni mwa watu ambao wanapaswa kufanya mabadiliko, basi napenda ujue sehemu muhimu ambapo mabadiliko uanzia. Unaweza kuwa labda unasema mabadiliko uanzia serikalini! Au mabadiliko uanzia kwa wazazi, ila kikubwa ni kwamba mabadiliko uanzia kichwani mwako.

Mabadiliko ya teknolojia yote unayoyaona yameanzia kichwani mwa MTU. Mabadiliko katika uwanja wa sanaa yameanzia kichwani mwa mtu.

Kwa hiyo rafiki, ukitaka kufanya mabadiliko, basi anza kubadilika kichwani mwako kwa fikra chanya, badililika kichwa mwako kwa kusoma vitabu, badilika kichwani mwako kwa kuwa na watu sahihi.
Mabadiliko yatakayofuata baada ya hapa, yatakuwa mabadiliko kweli kweli!

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X