Duniani kuna zawadi na vyeti vingi sana ambavyo vimewahi kutolewa. Kama umesoma shule kuanzia darasa la kwanza mpaka chuo basi utakuwa una rundo kubwa sana la vyeti. Lakini Swali ni je, vyeti hivi unavihitaji vyote? Utavitumia wapi?
Maana sasa hivi imefikia hatua hadi kuhudhuria semina watu wanatoa vyeti. Ukisoma vitabu watu wanakupa vyeti. Sasa hivi vyeti vyote vya nini?
Maana kubwa sana ya vyeti ni kutambua mchango/thamani yako kwa jamii. Kwa hiyo vyeti ni kama shukrani ila hupaswi kuvitegemea. Ikitokea watu wakakupa basi vipokee. Wasipokupa usivitafute kwa kulazimisha. Wewe kitu kikubwa sana unachopaswa kukazia ni kutoa huduma kwa jamii. Vyeti mtaani vinapimwa kwa kiwango cha pesa ulizoingiza au kiwango cha pesa ulizopoteza.
Na ukweli ni kwamba cheti kikuu ambacho unacho bure kabisa ni AKILI. Akili yako ina uwezo mkubwa sana. Kama utaitumia vyema itakutoa. Kitumie cheti hiki na cheti hiki ndicho unapaswa kutembea nacho kila mahali unapoenda. Hakitakutupa kama utaamua kukitumia vyema.
Soma Zaidi; Hivi Ndivyo Vitu Ambavyo Wanachuo Hawapendi Kufanya Ila Vinalipa Zaidi
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA