Hii Ndio Njia Bora Ya Kujiinua Mwenyewe


HII NDIO NJIA BORA YA KUJIINUA MWENYEWE

Hongera sana  rafiki kwa zawadi ya kipekee sana. Hii ndio siku iliyoandaliwa kwa ajili yako. Ifurahie na kuhakikisha unaitumia vyema kabisa.

Kila siku ni siku yako wewe kuhakikisha unakuwa bora sana kuliko jana. Yaani kujiinua.  Unapaswa kujiinua kwa vitendo, maneno, na wajibu, shughuli zako unazotimiza kila siku. Ila kama unataka kujiinua zaidi basi wasaidie wengine kuinuka juu zaidi.

Hii ndio njia ya uhakika ya wewe kuinuka. Ndio maana Wakenya wana usemi unaosema kwamba, “ukitaka kwenda kasi basi tembea peke yako, ukitaka kufika mbali tembea na watu”. Hii ndio kusema kwamba ukitaka kuinuka zaidi, basi wainue wengine zaidi.

Nakubaliana na Zig Ziglar ambaye falsafa ya maisha yake imekuwa chini ya msingi unaosema kwamba “unaweza kupata chochote kile unachohitaji kama utawasaidia watu kiasi cha kutosha kupata kile wanachohitaji”. Maneno haya ni ishara tosha kwamba zigler anapenda tuwainue watu wengine ili na sisi tuweze kuinuka zaidi na kusonga mbele. Kwa hiyo, rafiki yangu, kazi ya kufanya leo. Anza kutafuta namna ya kuwainua watu wengine. Ukiwainua watu wengine, kwa hakika utainuka juu zaidi.

Namalizia kwa kusema kwamba upendo wa kweli unauonesha pale unapoamua kuwasaidia wengine.

soma Zaidi; KONA YA SONGAMBELE; Zaeni Mkaongezeke

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X