Hili Ndilo Wazo Kubwa Sana Kuwahi Kutokea


Duniani kumekuwa na mawazo makubwa ambayo yameweza kubadili mwonekano wa dunia hii. Wazo la kuweka ndege angani lilikuwa ni wazo kubwa sana ambalo kiukweli mpaka sasa Kila mtu ni shuhuda kwamba limebadili mwonekano wa uso wa dunia. Wazo la kujenga ghorofa lilikuwa ni wazo kubwa sana ambalo kila anayeona jengo aina ghorofa leo hii lazima tu afutahi.
Wazo la kupata umeme ni wazo miongoni mwa mawazo mazuri sana ambalo linastaajabisha.

Ila leo hii napenda kukushirikisha wazo bora sana kuwahi kutokea kwenye dunia hii ambalo unapaswa kuwa nalo. Na wazo hili sio jingine bali ni wazo la KUSAMEHE.
Kusamehe ni wazo la kipekee mno kuwahi kutokea.

Labda utakuwa unajiuliza mbona kusamehe kunonekana kama kitu kidogo ambacho hakina maana. Nipende kukwambia kwamba sio kweli.
Kusamehe ni boonge la wazo. Unaposamehe maana yake unasahau yote ya zamani.
Unaposamehe unauachia moyo wako Uhuru.
Unaposamehe unajipa nafasi ya kuweka akili yako katika mambo makubwa ya sasa huku ukiachana na ya zamani.

Huu ndio muda wako kuachana na vinyongo. Huu ndio muda wako wewe kufurahi na kila mmoja. Kusamehe ni wazo kubwa sana.

Samehe kila unapokosewa. Samehe ili uishi kwa uhuru

Soma Zaidi: Liwezekanalo Leo Lisingoje Kesho

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X