Huu Ndio Upenyo Ambao Unapaswa Kuutumia Kusoma Vitabu


Hongera sana rafiki kwa zawadi ya siku hii ya kipekee sana. Hii ndio siku ambayo unapaswa kuitumia kuhakikisha kwamba unafanya makubwa sana.

Kati ya visingizio vya watu wengi sana kuhusu kusoma vitabu ni kwamba hawana muda.
Leo hii napenda nikupe upenyo mdogo ambao utautumia kusoma vitabu kila siku. Na upenyo huu upo kwenye muda wa ziada wa siku yako.

1. Muda ambao unakuwa safarini. Huu ni upenyo mzuri ambao unaweza kuutumia.
2. Muda ambao unakuwa unafanya mazoezi unaweza kusikiliza kitabu kilichosomwa. Utafaidika sana.
3. Muda ambao unakuwa unasubiri huduma sehemu fulani, pia ni muda mzuri wa kuutumia kusoma kitabu.
4. Muda ambao unakuwa haufanyi kazi ambayo inahitaji akili yako zaidi. Huu pia ni muda wako mzuri wewe kuutumia kusikiliza kitabu wakati unaendelea na shughuli hiyo ambayo haiitaji akili sana. Mfano wakati unapika.

Unaona eeh! Hapa ndipo ulipo upenyo ambao unaweza kuutumia kila siku kufanya makubwa, rafiki yangu. Ndio upenyo unaoweza kuutumia kusoma vitabu.

SOMA ZAISI;  UCHAMBUZI WA KITABU; THE 5 AM CLUB, Miliki Asubuhi Yako, Miliki Maisha Yako

Asante sana,
Tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
($ongambele)
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X