Kama Unafanya Kitu Hiki Basi Usitegemee Kupata Kile


Mbele yetu tena ni siku nyingine, nzuri na ya kipekee sana. Tunaenda kuhakikisha kwamba leo tunafanya kitu ambacho kitatusogeza mbele kwenye malengo yetu. Pia leo tunaenda kuhakikisha kwamba tunayafanya maisha ya mtu yeyote ambaye tutakutana naye, kuwa bora zaidi. Hii ndio siku njema ambayo tunaenda kuitumia.

Leo napenda kusema kwamba kama unafanya kitu fulani ukitegemea kupewa kitu fulani papo hapo. Basi afadhali achana nacho. Kama  unalima ukitegemea kupewa tuzo siku moja, basi wewe hujawa tayari kufanya hivyo.
Kama unafanya biashara ili siku moja uje usifiwe. Usiposifiwa utaumia sana.

Na hapa sio sehemu nzuri sana ya kujenga misingi yako ya kibiashara.

Msukumo wako katika kufanya kazi, kujituma usitegemee kupewa kitu cha kupongezwa ili usonge mbele. Maana isipotokea utaumia sana.

Msukumo wako wa kufanya kazi, utoke kwenye kwa nini zako. Kwa nini zako ni msukumo tosha wa kukufanya wewe ufanikiwe. Na unapaswa kuwa na kwa nini kubwa ambayo inakusukuma sana wewe kuhakikisha unafikia mafanikio makubwa.

Soma Zaidi: TAFAKARI YA WIKI:Elimu Ya Chuo Haitoshi, (Kitu Kimoja Unachopaswa Kuambatanisha Na Elimu Ya Chuo)
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X