Kitu Kikubwa Unachoweza Kufanya Juu Ya Ndoto Yako Kuu


Safari ya maisha inahusisha mambo mengi sana. Katika safari hii kuna watu wana kusudi kubwa ambalo wanapaswa kulitimiza na kuna watu wenye ndoto kubwa mno. Ndoto ni picha kubwa ya kesho yako ambayo unaijenga leo.
Ndoto ni jambo kubwa sana ambalo linakufanya usilale (halikupi usingizi) mpaka utakapokuwa umelitimiza.

Kutokana na ukubwa wa ndoto ambazo watu huwa wanazo, hivyo hakuna mtu kwenye historia ya kukamilisha ndoto yake kwa siku moja. Ndoto huchukua muda. Kutimia kwake huhitaji kuwekeza muda, akili, pesa, na rasilimali nyingine nyingi.

Sasa leo nikijua kwamba na wewe una ndoto kubwa sana, ninakuletea njia nzuri ya kuweza kukamilisha ndoto yako. Maana kuna watu wengi kutokana na ukubwa wa ndoto zao huwa hawatimizi ndoto zao.  Na njia hii ni wewe kuhakikisha unafanya jambo dogo kila siku kuhakikisha kwamba unaelekea ndoto yako kuu.

Rafiki yangu, kama una ndoto kubwa. Anza kuitekeleza kidogo kidogo kuanzia leo. Kamwe usisite kutekeleza ndoto yako kwa sababu ya ukubwa wake.

Anza kuitimiza kwa kutumia rasilimali ulizonazo. Fanya kinachowezekana mwisho wa siku utajikuta umeweza kuitimiza ndoto kwa ukubwa mno.

Soma ZaidiIfanye Dunia Ijue Kwamba Kuna Mtu Huyu Ndani Ya Dunia Hii

:


Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X