Mambo Matano (05) Unayoweza Kufanya Ukiwa Katika Mazingira Yanayokufanya Usijiamini


Moja kati ya vitu muhimu sana ambavyo unahitaji  katika maisha yako basi ni kujiamini. Kujiamini katika kazi unayofanya.
Kujiamini katika kile unachoongea
Kujiamini unapokuwa na watu n.k

Ubora Wa kujiamini ni kwamba unaonekana kwa macho. Yaani mtu anaweza kukuona kabisa na kukwambia kwamba hujiamini. Hii ni kutokana na tembea yako, ongea yako na mwonekano wako.

Sasa leo napenda nikushirikishe vitu vichache sana ambavyo vitakufanya siku zote uishi kwa kujiamini.

1. Hakikisha unavaa vizuri. Huwezi kujua utakutana na nani ukitoka chumbani kwako. Hivyo hakikisha unavaa nguo ambazo hazitakufanya ujusikie vibaya ukiwa na watu na hivyo kukupunguzia kujiamini kwako.

2. Usitembee wala kukaa na watu ambao wanakuambia maneno hasi ambayo yatakupunguzia kujiamini.

Soma Zaidi; Watu Sita Waliokuzunguka

3. Jikumbushe mambo madogo ambavyo umewahi kufanya kwa uzuri wa hali ya juu sana.

4. Sikiliza vitabu au soma vitabu vinavyokuongezea maarifa na ujasili wa kuchukua hatua.

5. Achana na mambo ya zamani. Weka nguvu yako katika kutimiza kazi hii ya leo au sasa hivi

Soma Zaidi; Matendo Hutibu Uoga

Ndimi,
Godius Rweyongeza
($ongambele)
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X