Mwandikie Mtu Huyu Barua Ya Kurasa Mbili Leo


Naam rafiki yangu. Siku zinazidi kusogea Mbele na maisha yanazidi kuwa bora zaidi. Tangu mwaka huu umeanza kuna hatua ambazo umekuwa unapiga kila siku. Inawezekana hatua hizi ni ndogo sana ila ni muhimu sana maana mafanikio makubwa sana huwa ni muunganiko Wa vitu vidogo vidogo ambavyo tunaviunganisha kila siku. Mwisho wa siku muunganiko wa vitu ndivyo huleta mafanikio makubwa sana.

Sasa leo kutokana na mafanikio haya madogo madogo ambayo umekuwa unafanya napenda ujiandikie BARUA ya kurasa mbili kujishukuru.
Katika BARUA hii jipongeze kwa hatua ambazo umekuwa unachukua.
Katika BARUA hii andika hatua ambazo umechukua
Na mwisho kwenye BARUA hii jikubali, kubali vipaji vyako na upekee wako.

Najua katika maisha yako utakuwa umewahi kuandika barua, ila hujawahi kujiandikia barua mwenyewe. Sasa leo jiandikie barua mwenyewe.

Soma Zaidi; Vitu Vitano Vinavyoharibu Ubunifu Wa Watanzania

Nakutakia siku njema sana.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X