NANI ATALIA UTAKAPOKUFA?


Katika kitabu cha WHO WILL CRY WHEN YOU DIE kuna sentensi moja ya kutafakariaha sana. Mwandishi wa Kitabu anaanza kwa kusema kwamba, “ulipozaliwa ulilia wakati waliokuwa wamekuzunguka wakishangilia, Unapaswa kuishi maisha kiasi kwamba utakapokufa watu walie huku wewe ukishangilia”.

Kauli hii sio kauli ndogo hata kidogo. Ni kauli iliyoshiba kweli kweli. Kauli hii inatufanya Mimi na wewe tujiulize tutaishije ili siku tutakapokufa watu walie huku tukifurahi?

Soma Zaidi; Umekufa Mwaka Gani?

Wakati tukijiuliza swali hilo hili mwandishi huyo huyo katika Kitabu cha THE SAINT, THE SURFER AND THE CEO (2013) anatupatia sehemu ya kuanzia kujihoji.
Anasema kuna maswali matatu ambayo tunapaswa kujiuliza Kila siku, kiasi kwamba tukifika mwisho Wa maisha yetu tutakuwa tunajua waziwazi kwamba tumekuwa watu Wa mchango mkubwa sana kwenye dunia hii. Maswali haya ni:
Je,nimehudumia vyema?
Je,nimependa ipasavyo?
Je,nimeishi kwa viwango vya juu?

Maswali haya yatakufanya uishi Kila siku badala ya kufa Kila siku maana, “kuna watu wanakufa wakiwa na umri wa miaka 20 huku wakisubiri kuzikwa wakiwa na umri wa miaka 80″ kama ambavyo anadokeza Robin Sharma.

Maswali hayo matatu naona kama yanatueleza kujua kwamba watu hawatalia  siku ya kifo chako kwa sababu tu wamelia. Ila watalia kwa sababu ya mchango wako.
Kwa hiyo ukijiuliza, je,nimehudumia vyema? Utakuwa unainua viwango vyako wewe kama wewe. Majibu ya swali hili yatakufanya ujue ni wapi bado hujaweka thamani na hivyo kukufanya uweke thamani zaidi hapo. Hii ndio kusema kwamba  swali hili linatupa jibu la kwanza la swali letu la Leo. Swali letu linauliza ni nani atalia utakapokufa?
Jibu la kwanza kabisa ni watu ambao uliwahudumia wewe kwa viwango vya juu.
Watu ambao uliwapa thamani kubwa sana katika kazi zako.
Watu ambao kila ulipokuwa ukikutana nao ulikuwa huwaachi walivyo bali ulikuwa unawafanya wasogee kwenye viwango vingine.

Ebu sasa tulijadili swali letu la pili, linalosema kwamba Je,nimependa ipasavyo?
Hili pia ni swali ambalo Unapaswa kujiuliza kila siku. Mwisho  wa maisha watu huwa wanakumbukwa kwa ukarimu na upendo waliokuwa wakiutoa. Kwenye msiba hakuna mtu ambaye huwa anasema kwamba Fulani, alikuwa tajiri, alikuwa na maduka, alikuwa ng’ombe. Watu huwa wanakumbuka viambata vya upendo.

Na hapa upendo unaoongelewa sio upendo wa mke na Mme. Kuna aina nne za upendo unaoongelewa hapa
>>kujipenda mwenyewe
>>kuwapenda wengine
>>kuupenda ulimwengu
>>kuipenda familia yako.
Upendo wako unaoutoa ndio utawafanya watu walie au wasilie.

Na hivyo kwa kumalizia kipengele hiki ukijiuliza Je,nimependa ipasavyo? Swali hili litakupa jibu la SWALI LETU KUU, linalosema, NANI ATALIA UTAKAPOKUFA

Kitu cha Mwisho tunachojadili Leo ni swali linalosema, je,nimeishi kwa viwango vya juu?
Kujiuliza swali hili kunatupelekea kutumia vipaji vilivyo Ndani yetu, uwezo tulio nao. Swali hili linatufanya tukazane kuwa bora zaidi ili walau tuweze kutumia nusu ya ubongo wetu.

Watu watakaonufaika na  vipaji, ujuzi na uwezo wetu basi watu hawa pia watakuwa miongoni mwa watu watakaolia utakapokufa.

Narudia tena kukuuliza,  Ni je, nani atalia utakapokufa?

Soma Zaidi; Fanya Haya Ili Uishi Milele

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X