Kwa siku mwanaume anasemekana kuongea maneno yasiyopungua 7,000 huku mwanamke akiongea maneno zaidi ya elfu 21. Wakati kauli na maneno yaliyo mengi yanayoongelewa mara nyingi huwa ni stori za kawaida, unapaswa sasa kubadilisha na kuanza kuongea kauli za kishujaa. Na leo hii nakuletea kauli moja muhimu sana ambayo ni ya kishujaa ambayo unapaswa kuitamka kila siku. Kauli yenyewe ni hii hapa,
“Nitakuwa king’ang’anizi mpaka nishinde. Nimekuja duniani kushinda wala kushindwa sio sehemu ya maisha yangu. Mimi sio kondoo ambaye nasubiri kuongozwa na mchungaji. Mimi ni simba, nakataa kata kata kutembea, kuongea na kuishi na kondoo. Nitakuwa king’ang’anizi mpaka nishinde”.
Ebu iandeke kauli hii sehemu. Isome na kuirudia kila iitwayo asubuhi, mchana mpaka jioni.
Nakutakia wakati mwema sana
Soma Zaidi: Hii Ni Kauli Unayopaswa Kuiepuka Maishani Mwako
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA