Hii Ndio Orodha Ya Vitabu Vya Kipekee Sana


1. KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI

Kabla ya kuandika kitabu hiki kulikuwa na maswali mengi ambayo nilihitaji kupata majibu yake.

Nilijiuliza. Hivi kwa nini katika jamii kuna watu ambao ni Matajiri na wengine ni masikini?
Kwa nini wengine wamefanikiwa huku wengine wanahangaika? Je, kwa nini baadhi ya watu wana mahusiano mazuri wengine mahusiano yao ni mabaya?
Kwa nini baadhi ya ndoa hudumu miaka 25, 50 na zaidi huku wengine wakiachana ndani ya siku chache?

Kiukweli maswali haya yalinisukuma kutafuta na kufanya utafiti wa kina sana.

Niligundua kwamba kuna vitu ambavyo Matajiri, watu wenye mahusiano mazuri na watu ambao wamefanikiwa katika fani mbali mbali (Iwe ni ujasiliamali, elimu, biashara n.k) wana sifa za kipekee sana.

Watu hawa wana tabia ambazo wanaziishi ambazo zinawafanya kuwa watu wa pekee na hivyo kuwapa mafanikio makubwa.

Kwa upande mwingine watu masikini na ambao hawajafanikiwa hawaishi tabia hizi. Yaani  kwao maisha ni bora liende tu.

Na tabia hizi kadri unavyozidi kuzikosa ndivyo unavyozidi kujinyima nafasi ya kufanikiwa na kufikia hatua kubwa sana.

Hivyo niliamua kuandika kitabu chenye tabia hizi ambazo Unaopaswa kuziishi kila siku. Tabia hizi zitakutoa sifuri MPAKA kwenye KILELE cha mafanikio kadri utakavyo  wewe, endapo utaziishi tabia hizi.

2. TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA.

Watu wengi sana wamekuwa wakilalamika kwamba Afrika ingekuwa ni nchi tajiri sana, kama isingetawaliwa na wakoloni. Wengine wanasema kwamba serikali haiwajali kabisa ndio maana hawajaweza kufikia hatua kubwa ya kimafanikio maishani.

Katika kitabu hiki cha TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA utakutana na kitu cha tofauti kabisa. Yaani utaanza kuyaona maisha kwa jicho la kipekee ambalo binafsi naliita jicho la dhahabu.

1. Utajua kwamba sehemu tajiri sio kwenye migodi ya madini kama ambavyo wengine wanafikiri, au kwenye machimbo ya gesi Mtwara. Sehemu kuu yenye utajiri makubwa sana karibu na wewe.

2. Utagundua kwamba maisha ni wajibu wako. Ukishinda ni juu yako, kushindwa pia kupo juu yako.

3. Mafanikio yanaambatana na gharama. Unapaswa kulipa gharama, ila sasa cha kushangaza gharama hii sio pesa!

3. Mitaji mkubwa mitatu ya kuanza kitu chochote unayo. Na hakuna mwingine wa kukunyanganya mitaji hii. Je, ungependa kuijua mitaji hii?

Hayo machache sana na mengine mengi mno yapo kwenye kitabu cha TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA.

3. NYUMA YA USHINDI

Kitabu cha tatu ni kitabu cha NYUMA YA USHINDI.

Kuna nini katika kitabu hiki?

Tuanze hivi,
Watu wengi sana wakiona MTU aliyefanikiwa basi moja kwa moja wanaanza kusema “unamwona mtu fulani yaani aligusa tu, mambo yakajipanga”. Hii ndio kusema kwamba mafanikio ya watu wengi yanahusishwa na bahati. Ila huo sio ukweli.

NYUMA YA USHINDI Kuna kushindwa, kushindwa, kushindwa. Watu ambao unawaona wanag’aa leo. Ni watu ambao wamepitia changamoto nyingi sana za kimaisha kuanzia utotoni mpaka hapo walipo. Kwa hiyo mafanikio yao sio bahati, Bali ni juhudi, uvumilivu, malengo makubwa, hatua kubwa, na mambo mengine kama ambavyo yameelezwa kwenye kitabu cha NYUMA YA USHINDI.

4. MAMBO 55 KABLA YA KUANZISHA BIASHARA

Hiki ni kitabu cha nne.
Watu wengi hupenda KUANZISHA BIASHARA ndogondogo kwa kubwa. Ila huwa hawajui ni mambo gani ya kuzingatia.
Nimeandaa mambo 55 ambayo unapaswa kuyazingatia kabla ya kuanzisha BIASHARA yoyote ile.

5. JINSI YA KUIBUA UBUNIFU ULIO NDANI YAKO

Kila MTU ni mbunifu. Na mbegu za ubunifu zipo ndani yetu. Mbegu hizi zinasubiri kupata vitu muhimu sana vya kuziwezesha kukua kama ilivyo mbegu ya kawaida ya mhindi.

 Ila tofauti pekee kati ya mbegu ambayo ipo ndani yetu na mbegu ya mhindi au maharage ipo kwenye mazingira muhimu yanayohitajika kwa mbegu zilizo ndani yetu kukua.
Mbegu ya kawaida ya mhindi inahitaji, maji, hewa na udongo kuota.

Ila mbegu iliyo ndani yako haihitaji, maji hewa na oksijeni ya kawaida. Kuna vitu zaidi ya 30 ambavyo mbegu ya ubunifu wako inahitaji.
Vitu hivi vyote nimevieleza kwa undani kwenye kitabu changu cha JINSI YA KUIBUA UBUNIFU ULIO NDANI YAKO.

KARIBU SANA.
Hii ndio orodha ya VITABU vyangu vilivyopo sokoni kwa sasa.

Vitabu vine kati ya vitano tajwa hapo juu, vinapatikana kwa nakala tete (soft copy). Na kitabu cha NYUMA YA USHINDI pekee ndicho kinapatukana kwa njia zote mbili nakala tete (soft copy) na makala ngumu (hard copy).

Bei za vitabu,
1. KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI tsh.10,000/-

2. TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA tsh. 10,000/-

3. NYUMA YA USHINDI tsh. 5,000/-

4.  MAMBO 55 YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZISHA BIASHARA tsh. 5,000/-

5.JINSI YA KUIBUA UBUNIFU ULIO NDANI YAKO tsh. 7,000/-

 karibuni sana

Bei ya jumla. Kama utanunua vitabu vyote kwa pamoja, kutakuwepo punguzo LA sh. 7,000/- hivyo utaweza kupata vitabu hivi kwa sh.30,000 badala ya 37,000/-
Karibuni sana.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X