Hii Ndio Tatu Mzuka Ambayo Hupaswi Kukosa Kuicheza


Kwa siku za hivi karibuni kumekuwepo na wimbi kubwa sana la uchezaji Wa michezo ya kubahatisha. Kitu hiki kimewafanya vijana kwa wazee wajihusishe na michezo hii ili kupata utajiri wa haraka.

Kinachotokea kwenye michezo hii ni kwamba mtu anajikuta anapoteza sana pesa zake kila akicheza.

Sasa rafiki yangu kwa kuwa nakujali sana, ningependa nikushirikishe tatu mzuka nzuri sana ambayo utapaswa tu kuiheza maishani mwako.

Tatu mzuka hii ni kuwapa watu wanachohitaji. Hii ni tatu mzuka ya kipekee sana. Watu watakuwa tayari kuja kukulipa kwa sababu kuna huduma unatoa na wao wanaihitaji.

Hii jiulize kila siku unaenda kununua vocha! Kwa nini?  Kwa sababu unapaswa kufanya mawasiliano. Au kiufupi ni kwamba unaihitaji.
Sasa na wewe tafuta sehemu ambapo utatoa huduma ambayo jamii inaihitaji ili uweze kucheza tatu mzuka ya kipekee sana.

Juu ya hili ZigZigler anasema, “unaweza kupata chochote maishani, kama utakuwa tayari kuwasaidia watu kupata kile wanachohitaji”.

Soma Zaidi: Unatumia Mabadiliko Ya Mitandao Ya Kijamii Na Intaneti Au Yanakutumia?

Nakutakia uchezaji mwema wa tatu mzuka hii mpya.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X