Kila umayemwona yuko juu kuna siku alikuwa chini. Kila jogoo anayewika kuna siku pia alikuwa kifaranga.
Suala hili linatupa mwelekeo mzuri kabisa wa kujua kwamba tunaweza kuwa tunayotaka kama tutaamua kuwa hivyo.
Lakini ili uweze kufikia kwenye kilele chochote kile mfano cha mlima lazima utokee chini. Na Unapaswa kupanda kuelekea juu. Unapokuwa umefika huko ndipo unapongezwa kama mshindi.
Na ili uweze kufikia juu kabisa kwenye kilele cha Mafanikio makubwa basi kitu kikubwa unachopaswa kuwa nacho ni ndoto yako kubwa. Ndoto kubwa ya kufikia huko. Sio kwamba vitu vingine vinatokea kwa ajali, bali vinatokea kwa sababu maalumu sana. Na hizi sababu zipo kwenye ndoto ya mtu. Ndoto ya kuona mbali.
Katika maisha unapaswa kuona mbali hamna jinsi. Kuona mbali sio kwa macho tu, lakini kwa fikra. Ndio maana tunaaswa kwa kuambiwa kwamba tunapaswa kulenga kulifikia jua, kiasi kwamba tukilikosa jua basi hata walau tuweze kuufikia mwezi
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA