Wale ambao leo hii unawaona wanafanya vizuri katika maeneo fulani ya maisha, basi kuna wakati walikuwa watu wa kawaida sana au hawajui kabisa kitu hicho. Ila baada ya muda kujitoa haswa sasa wamweza kufikia hapo unapowaona kiasi kwamba unatamani mafanikio yao. Juu ya hili wahenga wanasema kwamba “hata jogoo alianza kama kifaranga”
Kumbe kila unaowaona wanawika leo hii katika sekta kadha wa kadha iwe ni siasa, biashara, elimu, uchoraji na popote pale jua kuna siku walikuwa watu wa kawaida sana.
Soma Zaidi; Hii Ni Tatu Mzuka Ambayo Hupaswi Kukosa Kuicheza
Kilichowafanya kuweza kufanya mambo ya kipekee ni KUJITOA HASWA katika kazi zao. Yaani walijitoa bila ya kuacha nafasi ya kurudi nyuma. Yaani ilikuwa ni au wafikie mafanikio makubwa au wafe. Ilikuwa ni au wawe wafanyabiashara wakubwa sana au wafe.
Kwao ilikuwa ni kheri kufa ukiwa katika mapambamo kuliko kuliko kuishi miaka mingi ambayo haina mwelekeo.
Hivyo rafiki napenda nikwambie kwamba kama kuna kitu utapaswa kufanya maishani mwako basi ni KUJITOA HASWA.
Ukiamua, amua.
Ukifanya, fanya.
Soma zaidi; Haya Ni Mambo Ya Kipekee Usiyoyajua Kuhusu Biashara
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA
2 responses to “Hiki Ndicho Kitu Watu Waliofanikiwa Wanafanya”
Kazi nzur Godius
Asante.
Kazi nzur Godius
Asante.