Hiki Ni Kitu Ambacho Kitaimarisha Mahusiano Yako


Ikiwa ni siku nyingine kabisa rafiki yangu. Mwezi mpya na siku zinazidi kusogea mbele. Mwaka ambao hapo mwanzoni ulionekana ni mpya sasa upya wake hauonekani tena.

Leo hii napenda nikwambie kitu kimoja kitakachoimarisha mahusiano yako. Na hapa mahusiano ninayozungumzia ni mahusiano ya mme na mke, mahusiano ya kibiashara, mahusiano ya kindugu pamoja na mahusiano  yako na jamii yako.

Mahusiano haya unahitaji kuyaimairisha kabisa. Kitu kimoja kitakachokufanya uimairishe mahusiano haya ni wewe KUSIFIA. Unapaswa kujenga utaratibu mzuri wa kusifia watu waliokuzunguka. Sifia vizuri wanavyofanya, sifia mwonekano wao, sifia utendaji kazi wao, sifia tabia zao nzuri.
Muda mzuri wa kuona mazuri kwa mtu na kuyasema ni leo. Hivyo usisubiri hata sekunde moja bila kuchukua hatua.

Kitu hiki kimoja kitawafanya watu waongeze juhudi katika utendaji kazi wao. Kitakusogeza karibu na watu zaidi, kitafanya watu wapende sana kuwa karibu na wewe na kwa hakika kitaimarisha mahusiano yako. Anza kujenga tabia hii ambayo hukuwa nayo kabisa. Itakuinua zaidi ya ulivyokuwa unategemea.
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X