Hili Ni Jambo Ambalo Kila Mzazi Anapaswa Kumfundisha Mtoto Wake


Hongera sana rafiki kwa siku hii njema sana. Hii ni siku ya kipekee ambayo unapaswa kuitumia vizuri sana.

Watoto wanapozaliwa huwa hawajui kitu, bali huwa wanajifunza kila kitu kutoka kwa wazazi wao, jamii na mazingira yaliyowazunguka. Wazazi ndio watu wenye uwezo na ushawishi mkubwa sana kwa watoto maana vitu vingi sana vya kwanza maishani watoto huwa wanajifunza kutoka kwa wazazi wao. Miongoni mwa vitu wanavyojifunza ni pamoja na lugha wanayoongea. Kitu kikubwa ambacho wazazi wanapaswa kuwafundisha watoto wao ni UWAJIBIKAJI katika kazi.

Wazazi wanapaswa kuwafundisha watoto kufanya kazi na kujituma. Kujituma na kufanya kazi kwa watoto kunaanzia nyumbani na Mzazi maana ndiye mtu wa kwanza kabisa kumfundisha mtoto wake kazi. Hivyo basi

1. Nyumbani kuwepo na kazi ndogo ndogo ambazo watoto watashiriki kufanya.

2. Watoto waruhusiwe kuanzisha miradi midogo midogo  ambayo itawaingizia kipato.

3. Watoto waambiwe kazi ndio huleta thamani ya utu na hivyo wafanye kazi kujijenga wao wenyewe na kulijenga taifa.

Kama watoto hawatafundishwa kufanya kazi wakiwa wadogo, ukubwani tutakuja kushuhudia watu wanaokaa vijiweni kupiga tu stori. Ukubwani tutakuja kuona watu ambao wanaishia kulalamika kwamba hawakutengenezewa mazingira bora wakiwa wadogo. Na wazazi ndio watakuwa wa kwanza kulalamikiwa, hivyo basi samaki mkunje akiwa bado mbichi. Mtoto mlee vizuri kwa kumfundisha kuwajibika akiwa bado mdogo

SOMA ZAIDI; NIKIWA MKUBWA

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X