Chumvi ni miongoni mwa vitu ambavyo vimeanza kutumika tangu enzi na enzi. Yaani tangu mababu zetu enzi zile. Kikubwa kilichofanyika kwenye chumvi ni uboreshwaji wa kuitunza kwenye pakiti. Ila kazi chumvi ya mababu zetu na chumvi ya sasa ni ile ile.
Kazi yenyewe sio nyingine bali kuongeza radha katika chakula. Hii kazi ya chumvi. Sasa kazi hii sio tu kwa chumvi bali pia kwetu. Biblia inamwita mwanadamu chumvi (Mathayo 5:13). Hii ndio kusema kwamba mimi na wewe ni chumvi. Kwa hiyo sisi kama chumvi tunapaswa kuongeza radha katika chakula. Lakni je chakula chenyewe ni kipi?
1. Ni uliwengu. Tunapaswa kuifanya dunia na ulimwengu wote bora zaidi kupitia kazi zetu na ugunduzi wetu. Tunapaswa kukoleza radha ya dunia hii.
2. Ni watu tunaokutana nao. Kila siku tunakutana na watu wapya, tuhakikishe kila tunayekutana naye hatumwachi alivyo bali tunamfanya asonge mbele katika kazi zake. Awe mpya zaidi ya alivyokuwa.
Chumvi huwa ina tabia ya kuoza ikikaa lwa muda mrefu, yaani kupoteza uwezo wake wa kufanya kazi. Hali kama hii ikijitokeza basi jua kwamba chumvi hii haifai.
Vivyo hivyo kwetu sisi ambao ni chumvi ya dunia.
Usipotumia uwezo wako unaoza na kupotea. Kuthibitisha hili mwanasayansi Lamark aliwahi kusema kwamba kiungo cha mwili wa mtu kisipotumika hupoteza uwezo na mwisho hupotea kabisa. Je, wewe uoo tayari kuoza kwa sababu ya kutotumi uwezo wako?
Tukutane kwenye jukwaa la wanamafabikio
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA