IJUE KANUNI YA JUA NA JINSI YA KUITUMIA


Kwa kawaida jua huchomoza asubuhi na kuzama jioni.  Wakati jua linawaka huwa linapitia katika vipindi mbali mbali. Ambapo asubuhi huanza kuwaka taratibu, mchana ukali wa jua huongezeka wakati ila jioni ukali hupungua/ hufifia.

Jambo hili linafanana kabisa na maisha ya ukuaji wa binadamu.
Kuchomoza kwa jua asubuhi ni sawa na kuzaliwa kwa mtu.
Ukali wa jua mchana ni sawa na ujana, ambapo kijana anakuwa na nguvu kubwa sana ya kutimiza malengo na kufanya makubwa.
Kuzama pamoja na kufifia kwa jua ni sawa na uzee. Kipindi ambacho nguvu za mtu hupungua na utendaji kazi wake kushuka.

Hivyo basi nikushauri ukitumie kipindi cha mchana yaani kipindi cha ujana.
Kitumie vyema kipindi hiki maana una nguvu, afya njema na akili inafanya kazi kwa viwango vikubwa sana.
Zitumieni vyema sana siku hizi kabla hazijaja  siku ambapo nguvu zitaisha

1. Zitumie kuwekeza kwa sana.
2. Zitumie kujifunza kadri uwezavyo. Ukue kimwili na busara sio kuongezeka uzito tu.
3. Zitumie kutengeneza mtandao wa watu wengi wanaokufahamu ambao pia utawageuza wateja wako.

Kumbuka ukipoteza nguvu hizi hazirudi tena. Ukipoteza hata sekunde moja ndio hivyo, hairudi tena.

Soma Zaidi; TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA-68, tatizo hujajua kwa nini hujui

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X