IJUE KANUNI YA UJENZI WA GHOROFA NA HAKIKISHA UNAITUMIA


Kati ya vitu ambavyo vinashangaza sana ni ujenzi wa ghorofa. Ghorofa ni nyumba iliyojengwa ikiwa na vyumba juu yake. Sasa kinachotokea ni kwamba ujenzi wa ghorofa huanza kwa kuchimba msingi wake kwenda chini. Tena kadri ghorofa inavyokuwa ndefu zaidi ndivyo wajenzi wake wanashuka chini zaidi katika uchimbaji wake.
Kitu hiki kinatufundisha jambo kubwa sana katika maisha. Hii ndio kusema kwamba ukitaka kupanda juu katika maisha na mafanikio utapaswa kushuka chini. Na kadri utakavyotaka kupanda juu zaidi ndivyo utataka kushuka chini zaidi. Kama ilivyo kwa kuruka. Ukitaka kuruka juu zaidi sharti uiname chini kwanza ili uruke.

Sasa labda tujiulize kushuka chini huku maana yake ni nini?
1. Ni kuachana na baadhi ya vitu ambavyo ulikuwa umezoea na kuanzisha tabia mpya kwa ajili ya kesho yako.

2. Ni kupoteza baadhi ya vitu ambavyo sio muhimu kwa ajili ya kupata zaidi. Wakati wa ujenzi wa ghorofa wajenzi huondoa udongo kwanza. Hii ndio kusema kwamba udongo hauhitajiki. Hivyo unaondolewa ili viwekwe vitu vingine vya muhimu zaidi.

3. Ni kuambatana na vitu vipya ambavyo vitakufikisha kwenye kilele cha mafanikio. Wajenzi huondoa udongo na kuleta mawe, simenti n.k ili kujenga ghorofa. Na wewe kwenye maisha kuna vitu utapaswa kuondoa lakini pia kuna vitu utapaswa kuambatana navyo. Utapaswa kuambatana na usomaji wa vitabu, utapaswa kuambatana pia na marafiki chanya.

Soma Zaidi: NIMEZALIWA MSHINDI: IJUE KANUNI YA PASI NA HAKIKISHA UNAITUMIA

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


One response to “IJUE KANUNI YA UJENZI WA GHOROFA NA HAKIKISHA UNAITUMIA”

  1. Ni kweli, bw. God, hata katika vitabu vitakatufu tunaambiwa tusipendelee viti vya mbele, lakini Kama tuna kitu muhimu kwa jamii, basi jamii hiyo itatupeleka ktk viti vya mbele.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X