Unahitaji Kitu Kimoja Tu


Kama kuna kitu kimoja unapaswa kufanya maishani mwako basi ni kutafuta kitu kimoja na kuweka nguvu, muda, akili na uwezo wako wote hapo.

Kuna vitu vingi sana vya kufanya kila iitwayo leo, lakini je, vitu hivi vyote vinahitaji muda wako? Huhitaji kuhangaika na kila kitu kinachokuja mbele yako. Bali unapaswa kuwekeza nguvu na muda mwingi sana katika vitu vichache sana ambavyo vinakupa matokeo makubwa sana. Itakuwa bora zaidi kama kitakuwa kitu kimoja tu.

Ukifuatilia watu wengi waliofanikiwa kufanya mambo makubwa sio wale waliokuwa wanatanga tanga kila sehemu kwa kufanya kila kitu, bali ni wale ambao wamewekeza muda mwingi katika kazi chache au katika lengo moja tu maishani. Hivyo kila walichofanya kimekuwa ni kuendana na hilo lengo lao kuu maishani mwao.

Chukulia mtu kama Messi, sasa hivi kila kitu anachofanya ni kuboresha ujuzi wake wa kucheza mpira sio kitu kingine.

Au angalia mtu kama Nelson Mandela yeye kitu chake kimoja alichowekea mkazo maisha yake yote ilikuwa ni kukomesha ubaguzi wa rangi Afrika Kusini. Je, wewe kitu gani kimoja unaweka juhudi, nguvu na muda wako kila siku?
Ni kitu gani kimoja ambacho kinawasha moto wa ndani yako kila siku?
Kitafute kitu hiki!

Soma Zaidi; Hiki Ni Kitu Ambacho Kitaimaimarisha Mahusiano Yako

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X