DO OR DIE: Kitu Unachokihitaji Kuliko Kitu Kingine Chochote Maishani


Kitabu cha nyuma ya ushindi kipo kwa ajili yako. Tsh 5000/-

Siku za hivi karibuni kulikuwa na timu ya mpira wa miguu ambayo ilikuwa  inahamasisha wachezaji wake kwa kutumia kampeni ya FANYA AU KUFA (DO OR DIE). Kampeni hii imeonesha kuzaa matunda makubwa sana kwa timu husika.

Kampeni hii bado inaonekana kama kampeni inayoifaa timu iliyokuwa inaitumia tu. Watu wengine wameishia kuiongelea kwenye mitandao ya kijamii, vijiwe na kila kona ila wao kuitumia hawataki.

Labda  kwa haraka niseme na wewe unaihitaji kampeni hii. Tena inakufaa sana wewe zaidi hata ilivyokuwa inaifaa timu iliyoitumia.

Inakufaa kwenye biashara yako. Ukitaka kuongeza mauzo kwenye biashara yako basi wewe tumia kampeni ya FANYA AU KUFA.

Soma Zaidi: Hii Ni Sentensi Iliyonichekesha

Kwa nini fanya au kufa? Ni kwa sababu au utatangaza biashara yako ili kuwafikia wateja zaidi na hivyo kukua au utaacha kufanya hivyo kitu kitakachopelekea wewe kupunguza mauzo. Na kama mauzo yanapungua basi jua kwamba unakufa.

Ni au utafanya ubunifu kwenye biashara yako unaovutia wateja zaidi au utawaiga watu wengine na hivyo kuiua biashara yako.

Ni au utaamua kuongeza mtaji kwenye biashara yako ili ipanuke zaidi au utaamua kula hata faida inayopatikana kitu kitakachopelekea wewe kuiua biashara yako. Ndio maana nasema hivi, DO OR DIE unaihitaji wewe kuliko anavyoihitaji mtu mwingine yeyote.

Hata kama umeajiriwa utahitaji kutumia DO OR DIE kuliko mtu mwingine haswa kwenye zama hizi ambapo kazi nyingi zinazidi kufanywa na kompyuta, hivyo utapaswa kujitofautisha mwenyewe na kufanya mambo ya tofauti kiasi kwamba haiwezi kupatikana kompyuta yenye uwezo wa kufanya kazi ambayo wewe unaifanya.

Matumizi ya kipaji chako yawe ni DO OR DIE. Ni au unatumia kipaji kuleta tija kwenye jamii   au unakufa na kipaji chako.
Ni au unakitumia kipaji chako kukuinua wewe na  watu waliokuzunguka au unaacha kabisa.

Hivyo basi kuanzia leo, anza kutumia kampeni ya FANYA AU KUFA. Ukianza kazi usijihurumie kwa kusema nitafanya baadae. Hapo utapaswa kujiambia kwamba hapa kuna mawili. Ni au ninafanya ili niendelee kuishi au ninakufa.

Asante sana rafiki yangu. Tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


One response to “DO OR DIE: Kitu Unachokihitaji Kuliko Kitu Kingine Chochote Maishani”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X