USIDHARAU MTU KWA KUMWANGALIA TU


Katika maisha kuna watu na vitu vinanifurahisha sana. Kati ya watu wanaonifurahisha sana ni wajenzi, hasa wajenzi wa ghorofa. Wakianza kujenga wanachukua mabati wanazungushia eneo linalojengwa (tena muda mwingine mabati makuukuu).
Sasa wewe ukitoka huko na dharau zako unaweza kushangaa na ukacheka sana. Kumbe wenzako ndio wapo wanajenga kitu cha ghorofa.

Kitu hiki kitufanye tutafakari juu ya maisha ya kawaida ya kila siku. Ukimwona mtu ni kawaida usimdharau huwezi jua mtu huyo anapanga nini kwa wakati huo. Inawezekana wewe ukaona mabati chakavu kwa nje, kumbe mtu huyo kwa ndani anajenga kitu cha ghorofa. Inawezekana leo hii ukamwona mtu havai vizuri, kumbe jamaa ndio anajichanga kuanzisha biashara.
Unaweza kumshangaa kwamba jamaa haendi na fasheni kumbe mtu huyo ndio kwa wakati huo ana  mpango wa kuanzisha duka LA nguo za fasheni unazozipenda wewe.  Kamwe, usiendekeze dharau kwa kutumia mwonekano was mtu wa sasa hivi. Sehemu pekee unapopaswa kutumia dharau ni makaburini. Huko ndiko kuna watu ambao hawawezi kujishughulisha tena.

Soma Zaidi; IJUE KANUNI YA UJENZI WA GHOROFA NA JINSI YA KUITUMIA

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X