Aina Tatu Za Mahusiano Na Moja Inayokufaa Wewe


Hongera sana rafiki yangu mpendwa kwa zawadi ya siku hii nyingine njema sana. Hii ni siku ambayo ambayo unapaswa kuitumia haswa kwa sababu ya upekee wake. Lakini pia kwa upendeleo wako kuiona siku ya leo. Sio kila mtu ameweza kuiona siku hii njema mno.

Sasa tuje kwenye makala ya leo
Mahusiano yoyote yale, yawe ni ya kirafiki au kimapenzi kwa vyovyote vile tunaweza kuyagawa katika aina tatu.

Moja: Pale ambapo upande mmoja unakuwa unafaidika sana na mwingine haufaidiki kwa chochote. Yaani hapa inakuwa ni kama upande mmoja ni chambo wakati mwingine samaki anakula chambo. (Parasitism)

 Mbili; ni pale upande mmoja unapofaidika kutoka upande wa pili ila upande wa pili hauumii. (Commensalism)

Tatu; ni pale pande zote zinaponufaika na uwepo wa kila upande (mutualism). Hii ndio aina nzuri ya mahusiano.

Kwenye mahusiano yoyote ambayo upo jua kwamba yataangukia kwenye eneo mojawapo kati ya hayo. Kazi yako ni kuyatafuta mahusiano gani yanakuumiza na kuondokana nayo.

Kama umeona kuna mahusiano ambayo yapo kwenye aina ya kwanza na ya pili, basi achana nayo. Kazana kujenga mahusiano aina ya tatu.

Soma Zaidi; Hiki Ni Kitu Ambacho Kitaimarisha Mahusiano Yako Zaidi

Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X