Ukilinganisha na vile ambavyo tunapaswa kuwa watu wameamka nusu”, alisema Profesa James William kutoka chuo kikuu cha Harvard. Hivi kumbe kwa msingi huu profesa William alitaka kutwambia kwamba watu wana uwezo mkubwa sana ila hata nusu ya uwezo huo haijatumika hado. Daah inashangaza sana.
Kama wewe unasoma hapa basi utakuwa na ufahamu mzuri wa simu aina ya smartphone. Hiki ni kifaa chenye uwezo mkubwa sana. Inasemekana kwamba uwezo wa kifaa hiki ni mkubwa kuliko kompyuta ya kwanza iliyopeleka mtu mwezini. Ila sasa cha kushangaza watu wengi wanaitumia tu kupiga simu, kutuma meseji na kuingia mtandaoni. Kumbe hapa huhitaji mtaalam kukwambia kwamba unaitumia chini ya kiwango.
Sasa mfano huu ni kama wewe hapo. Kwa uwezo mkubwa ulio nao kiukweli unatumia kitu kidogo sana.
Chukulia pale unapoanza kufanya kazi na kuchoka. Ukijihisi kuchoka tu unaacha, ila hapo unaambiwa unakuwa umetumia asilimia 40 tu. Ukijisukuma zaidi ya hapo unaweza kufanya zaidi na kwa viwango vya zuu zaidi
Hivyo kuanzia leo ukijihisi kuchoka usiache kufanya. Jiambie kwamba mpaka Sasa nimetumia asilimia 40 tu ya uwezo wangu bado asilimia 60. Siku zote jikaze kuzitumia hizi asilimia 60. Ukiweza hata kutumia nusu ya uwezo wako basi utakuwa umepiga hatua kubwa sana.
Soma zaidi: GHARAMA YA KULIPA ILI KUPATA MATOKEO MAKUBWA
Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA